ZAIDI YA WANANCHI 800 WAMEPATIWA VIPIMO NA MATIBABU KUTOKA KWA MADAKTARI BINGWA. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, September 16, 2023

ZAIDI YA WANANCHI 800 WAMEPATIWA VIPIMO NA MATIBABU KUTOKA KWA MADAKTARI BINGWA.


Na  Bugoma Wa Bugoma.
Katavi

Zaidi ya wananchi 800 mkoani Katavi wamefikiwa na kupatiwa huduma za vipimo na matibabu kutoka kwa madaktari bingwa ambao wanatoka hospitali ya Benjamini Mkapa ambapo huduma hiyo imetolewa katika hospitali ya rufaa mkoani humo.


Crisencia Malango, Otana Muroya na Hamza Hongo ni baadhi ya wananchi waliofurahishwa kwa kupatiwa huduma hiyo ya madaktari bingwa ambapo awali walikua wanatumia gharama kubwa kufuata huduma hiyo ya madaktari bingwa.

Parason Mtasingwa ni daktari kiongozi kutoka hospitali ya rufaa mkoani Katavi amesema takribani wananchi 1000 wamefikiwa na madaktari bingwa huku zaidi ya 800 wamepatiwa matibabu ya madaktari bingwa huku Jeremia Mbwambo ambaye ni afisa mawasiliano kwa uma kutoka hospitali ya Benjamini Mkapa ameishukuru serikali kuendelea kujenga miundombinu bora katika sekta ya afya.


Taska Mbogo ni mbunge wa viti maalumu kutoka mkoa wa Katavi amewahakikishia wananchi wa mkoa huo kufanya jitihada za dhati ili madaktari hao bingwa waweze kurudi kutoa huduma za kibingwa katika mkoa huo kwani muda uliopangwa ulikua mchache.

Mbali na hayo Taska ameishukuru serikali kwa kuendelea kujenga miundombinu bora katika sekta ya afya sambamba na kununua vifaa tiba ambavyo ndio nguzo muhimu katika sekta hiyo.




No comments:

Post a Comment