BIL. 4 KUJENGA SOKO NA MAEGESHO YA MALORI - NZEGA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, October 18, 2023

BIL. 4 KUJENGA SOKO NA MAEGESHO YA MALORI - NZEGA


OR-TAMISEMI

Rais wa Jamhuru ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema Serikali italeta shilingi Bilioni 4 kaa ajili ya ujenzi wa soko na eneo la maegesho ya malori kwenye Halmashauri ya Nzega Mji, mkoani Tabora.

Mhe. Rais Samia ameyasema hapo leo tarehe 18.10.2023 baada ya kutembelea soko la Wamachinga Parking na kujionea changamoto mbalimbali zinawakabili wafanyabiashara wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani humo.

Amesema Mbunge wenu alilamika kuhusu soko nikamuambia Waziri wa TAMISEMI pekua kama kuna fedha, lakini nikasema bora nije nione na hapa niko mimi, Waziri wa TAMISEMI na Mbunge wenu nimeongea na wakinamama wawili watatu wamesema wakirekebishiwa tu mazingira patakaa vizuri hivyo tumeamua tuanze ujenzi wa soko hili.

“Tutaangalia kama kuna nafasi tunataka kutoa nafasi ya kupaki malori makubwa maana nimeambiwa huko Stendi yanaleta usumbufu hivyo tutaangalia michoro itakavyokua na kwa kuanzia tumetenga shilingi Bilioni 4 kwa ajili ya kuanza ujenzi’ alisisitiza Rais Samia.


Aliongeza “Wakati wa ujenzi mtatakiwa kupisha hivyo msiwe wakaidi, wanasema kujenga ni kubomoa hata nguo ili ishonwe lazima ikatwe kwanza, sasa na hapa itabidi pabomolewe pote hapa hivyo itabidi mkubali mpishe ili ujenzi uweze kuendelea.

Na mwisho amewataka Uongozi wa Halmashauri hivyo kuwapa kipaumbele wafanyabiashara waliopo hivi sasa mara Soko hilo litakapokamilika wapate kwanza wao maeneo ndipo wapewe na watu wengine.

Mhe. Dkt. Samia yuko katika siku ya Pili ya ziara yake mkoani Tabora.


No comments:

Post a Comment