Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Kamishna Benedict Wakulyamba ameipongeza Timu ya Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kutangaza utalii wa ndani na kupambana vilivyo katika michezo inayoendelea na kuiletea ushindi kwenye michezo mbalimbali iliyofanyika kwenye Mashindano ya 37 ya Shirikisho la Michezo la Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) yanayofanyika Mkoani Iringa.
Akizungumza leo mara baada ya kutembelea Timu hiyo katika Viwanja vya Chuo Kikuu cha Ruaha ambapo yanafanyika mashindano hayo, Kamishna Wakulyamba amewapongeza Viongozi wa Timu hiyo pamoja na wachezaji wote kwa kufanikiwa kuiletea Wizara Vikombe vya Ushindi na kutangaza Utalii.
Kwa Upande wa Mwenyekiti wa Klabu ya Wizara ya Maliasili na Utalii, Bi. Getrude Kassara amesema mashindano hayo yamewasaidia kwani Watumishi hao wameweza kufahamiana na watumishi wengine lakini pia imewatengenezea uimara katika utendaji kazi pindi watakapo rudi ofisini.
Naye Mratibu wa Timu hiyo,Bw. Leodger Kiwia amempongeza Kamishna Wakulyamba kwa kutembelea wanamichezo wa Timu hiyo huku akisisitiza kuwa suala hilo limewapa hamasa ya kushindana na liwewapa nguvu katika kuhitimisha michezo hiyo.





No comments:
Post a Comment