BAKITA LATAKIWA KUIBUA VYANZO VIPYA VYA MAPATO NA KUSIMAMIA MATUMIZI YA KISWAHILI FASAHA. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, October 12, 2023

BAKITA LATAKIWA KUIBUA VYANZO VIPYA VYA MAPATO NA KUSIMAMIA MATUMIZI YA KISWAHILI FASAHA.


Na Mwandishi Wetu - BAKITA

Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Gerson Msigwa ametembelea Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) na kuiagiza menejimenti ya Baraza kuibua vyanzo vipya vya mapato ikiwa ni pamoja na kuanzisha vituo vya Kiswahili jijini Dodoma na Arusha.

Katibu Mkuu Msigwa ameyasema hayo Oktoba 12, 2023 katika ziara yake ya kwanza tangu alipoteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa wizara hiyo, ambapo ameitaka kuanzisha kozi fupi kwa Waandishi wa Habari, Makatibu Muhtasi na Watanzania kwa ujumla.


“Hii ni ziara ya kutembelea taasisi ambazo ziko chini ya wizara ninayoiongoza ili nijue maendeleo yake na kubadilishana mawazo na viongozi wa taasisi", amesema Msigwa.


“Tutabidhaisha Kiswahili na tutasimamia Kiswahili fasaha kwa kuwa tunayo fursa ya kupeleka Kiswahili katika nchi zote duniani. Kati ya mambo yasiyofaa ni kuona vyombo vya habari vinaharibu lugha ya Kiswahili, tushirikiane na BAKITA kutumia Kiswahili fasaha kwani sisi ndio wa kushika bendera yetu na kuipeperusha lugha fasaha ya Kiswahili", amesema Bw. Msigwa.


Amelitaka BAKITA kuongeza jitihada za kutangaza lugha ya Kiswahili kwani ndilo jukumu lake la msingi.

No comments:

Post a Comment