DKT.MPANGO AWATAKA NGOs KUTOTUMIKA KAMA TARUMBETA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, October 5, 2023

DKT.MPANGO AWATAKA NGOs KUTOTUMIKA KAMA TARUMBETA


Na Okuly Julius-Dodoma

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Philip Mpango ameyataka Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kutokubali kutumika kama tarumbeta na Watu Wenye nia Ovu na wasioitakia Mema nchi,badala yake wahakikishe wanalinda na kutunza maadili ya Kitanzania.

Ametoa maelekezo kwa Kamati ya kudumu ya Bunge ya huduma za ustawi na maendeleo ya jmii kufanya uchambuzi wa mchango wa mashirika hayo na kuishauri serikali juu ya mwenendo na ufanisi wake.


Dkt.Mpango ametoa maagizo hayo Leo Oktoba 5,2023 Jijini Dodoma wakati akifunga jukwaa la mwaka la mashirika yasiyo ya kiserikali.

Nashauri kuanzishwa Kwa Tuzo hasi Kwa Mashirika ambayo hayafanyi vizuri katika utekelezaji wa majukumu yake.

"Mashirika yetu yasiyo ya kiserikali msikubali kutumika kama tarumbeta Kwa watu Wenye nia Ovu na nchi yetu na msikubali kutumika kama mlango wa Kupenyeza mambo ambayo yanakwenda kinyume na Maadili,sheria na Utamaduni wa Taifa letu,"amesema Dkt.Mpango

Pia Dkt.Mpango ameyashauri Mashirika hayo kuanzisha tuzo hasi Kwa Mashirika yanayofanya vibaya ili kuyakumbisha kuwa wanawajibu wa kuongeza jitihada katika utekelezaji wa majukumu yao.


Pamojaa na hayo Dkt.Mpango amezindua ramani ya kidigitali ya utambuzi wa mashirika yasiyo ya kiserikali.

Kwa upande wake Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt.Dorothy Gwajima amesema wizara anayoiongoza kupitia Ofisi ya msajili wa NGO's ina jukumu la kuratibu shughuli za mashirika hayo kwa upande wa Tanzania Bara ili kuhakikisha yanaleta tija kwa jamii.

Mwenyekiti wa Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Mwantumu Mahiza ameziomba mamlaka za mikoa na wilaya kufanya kazi kwa karibu na mashirika yasiyo ya kiserikali huku Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la mashirika hayo ametaja changamoto zilizopo ikiwemo mfumo wa mamlaka ya kodi kutokuwa rafiki.

No comments:

Post a Comment