Na Imma Msumba ;
Arusha
Kamati ya kudumu ya Bunge
ya Viwanda,Biashara ,Kilimo
na Mifugo imetembelea
mradi wa ujenzi wa bwawa
la umwagiliaji katika
shamba la wakala wa
mbegu za kilimo ASA katika
eneo la Ngaramtoni ambapo
kamati hiyo ilikuwa
ikiongozwa na Mwenyekiti
wa Kamati hiyo
Mhe.Mariam Ditopile
ambaye ni Mbunge wa Viti
Maalum kupitia Mkoa wa
Dodoma.
Akizungumza katika ziara
hiyo kwa niaba ya
mwenyekiti wa kamati hiyo
Ezra Chiwaleza ambaye ni
Mbunge wa Biharamulo
amesema wanampongeza
sana Rais wa Jamuhuri ya
Muungano wa Tanzania
Samia Suluhu Hassan kwa
kazi kubwa aliyoifanya na
kutoa pesa nyingi
anazoendelea kuwapatia
katika wizara ya kilimo
“kama tulivyoona mradi
huu wa ASA uliopo
Ngaramtoni kazi
inayoendelea ni kubwa
bwawa limechimbwa na liko
katika hali nzuri na kufikia
katika hatua ya umaliaziaji .
“Pia tumpongeze
mkandarasi anayefanya kazi
hii kazi inaridhisha kama
kamati tumefika hapa
tumeona kazi ni nzuri na
tunampongeza pia
mkurugenzi kwa kazi
kubwa anayoifanya “alisema
Kikubwa sisi tumewahasa
kwa yale ambayo wanaona
kwamba wanayaitaji kama
kamati ilikuweza kuifikia
ndoto ya Rais kwenye
kuwahudumia watanzania
wayalete kazi ya kamati
tunapokuja hapa hatuji
kama mahakimu tunakuja
kuona changamoto ambazo
wanazo watendaji hususani
taasisi ambazo ziko chini ya
wizara ili twende tukaseme
kwa niaba yao kama kamati
inayosimamia wizara hizi ili
pesa inayoitajika iweze
kupatikana kwaajili ya
kufanya utekelezaji.
Kamati imeridhika na
miradi inayoendelea hapa
miradi ni mizuri tunazidi
kuwauunga mkono kwahiyo
wafanye haraka kwa wale
ambao wanayo ili kamati hii
chini ya mwenyekiti wetu
tuone ni jinsi gani
tukashauri serikali ili yale
ambayo yanaitajika kwaajili
yakuweza kuongezea nguvu
yaongezewe nguvu ili
waweze kuwahudumia
watanzania maana kazi
inayofanywa na ASA ni
kuhakikisha watanzania
wanapata mbegu bora
ilipale unapolima eneo dogo
uweze kuzalisha kwa wingi.
“Sasa kama kazi hii
haitafanyika maana yake
watanzania wataumia
watakuwa wanatumia
mbegu zilezile za kienyeji
unalima hekari ishirini
unavuna kidogo ila
aliyelima hekari tano
anavuna zaidi yako
wewe”aliongezea
Naye Naibu waziri wa
kilimo Ernest Silinde
ameeleza kuwa wizara
inafanya kazi kwa karibu na
kamati hiyo na inajukumu
la kupitisha fedha na moja
ya jukumu lao ni kuangalia
maendeleo ya mradi na
kushauri kwa kutoa
mapendekezo kulingana na
kile walichokiona.
“Niwahakikishie kamati ya
bunge kwamba maoni yao
ushauri wao wote walioutoa
sisi kama wizara
tumeyapokea
na tutakwenda
kuyafanyia kazi kama
ambavyo tumekuwa
tukifanya hivyo mara kwa
mara”
Hata hivyo nipende
kuwaeleza watanzania
mashamba haya ni kazi
nzuri inayofanywa na Dkt.
Samia hayani maono yake ni
maoni ya Ilani ya chama cha
mapinduzi maono haya
yanayofanyika hapa
yamekusudia jambo moja
kuongeza uzalishaji wa
mbegu bora hapa nchini
kwasababu tunahitaji
mbegu bora na zauhakika
katika muda wote wa
msimu.
"Tumekuwa na changamoto
ya mbegu kwa muda mrefu
tumekuwa tukitumia fedha
za kigeni kuagiza mbegu
nchini kwahiyo tukiongeza
uzalishaji maana yake
tutapunguza matumizi ya
fedha za kigeni nje ya nchi
mpaka kufikia 2030 tuwe
tumeondoa uhaba wa mbegu nchini." Aliongezea
Kwaupande wake Mkuu wa
Mkoa wa Arusha John
Mongella,ameiomba kamati
hiyo kuhakikisha mashamba
11 yawawekezaji
yaliyorudishwa serikalini
takribani miaka mitano
iliyopita wayafanyie
mpango
iliyaweze kurudi katika
wizara ya kilimo ili
yakaendelezwe kwani soko
la dunia ya sasa linataka
mbogamboga na maua
“mwenyekiti wa kamati
shamba moja lilikuwa
linaajiri zaidi ya
wafanyakazi elfu moja
asilimia 90 ya wafanyakazi
hao walikuwa ni wanawake
na vijana ”alisema

No comments:
Post a Comment