TANZANIA YAKABIDHIWA KIJITI UENYEKITI BODI YA AICAD - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, October 5, 2023

TANZANIA YAKABIDHIWA KIJITI UENYEKITI BODI YA AICAD


Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo leo Oktoba 5, 2023 amekabidhiwa Uenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Afrika (AICAD) inayohusika kujengea uwezo Vyuo Vikuu na Jamii katika masuala mbalimbali ikiwemo Kilimo, maji na kuongeza thamani.

Prof. Nombo anapokea nafasi hiyo kutoka Kenya kwa ajili ya kuongoza kwa miaka miwili kuanzia mwaka 2023.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa Prof. Nombo ameshukuru na kupongeza Uongozi uliopita kwa kazi nzuri, huku akisisitiza nia yake ya kusimamia malengo ya Taasisi hiyo kikamilifu.

‘’Namshukuru Mwenyekiti aliyemaliza muda wake kutoka Kenya, hakika umeiongoza Taasisi hii vizuri, mmetusaidia kufika hapa tulipo. Pia naipongeza na kuishukuru menejimenti ya Taasisi akiwemo Mtendaji Mkuu Prof. Dominic Byarugaba amefanya kazi nzuri kuibadilisha taasisi.

Ameongeza kuwa ni heshima kubwa kwa Nchi na kwake kupata nafasi ya kuiongoza Taasisi hiyo muhimu na ameahidi kuwa atajitahidi kutekeleza majukumu yake ya kuongoza Bodi kusimamia taasisi kufikia malengo.

Akizungumzia umuhimu wa Taasisi hiyo Prof. Nombo amefafanua kuwa AICAD kupitia ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA) kuanzia mwaka 2012 imefanya makubwa sana, mathalani hapa Tanzania imesaidia kuibuliwa kwa Teknolojia mbalimbali.

‘’Mfano wa teknolojia iliyoibuliwa kupitia ufadhili wa JICA ni namna ya kujenga nyumba kwa gharama nafuu, ukienda Chuo cha SUA na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam utakuta teknolojia hiyo inatumika sana kuhakikisha tunajenga nyumba kwa kutumia gharama nafuu’’. Alinena Prof Nombo.

Akiwasilisha taarifa ya makabidhiano kwa niaba ya Mwenyekiti aliyemaliza muda wake, Dr. David Matene ameishukuru Bodi kwa kumpatia ushirikiano katika kipindi chote alichoongoza, pia ameahidi kuendelea kushirikiana na Mwenyekiti mpya kuendelea kuijenga na kiimarisha taasisi hiyo katika kutekeleza majukumu yake.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya AICAD Prof. Dominic Byarugaba amempongeza Prof. Nombo kupokea mamlaka hayo makubwa na yenye malengo mtambuka na amevitaka Vyuo Vikuu kuzalisha Wahitimu mahiri na wabunifu ili waweze kutatua changamoto katika mbalimbali katika jamii.


No comments:

Post a Comment