Viongozi wa Kamati ya Siasa ya  Kata ya Kilimani Jijini Dodoma pamoja na Wajumbe wa  Sekretarieti   ya kata ya Kilimani    Wamefanya ziara yakukagua Mradi wa Ujenzi wa Shule  ya Msingi  unaotekelezwa katika Mtaa wa chinyoyo kata ya Kilimani na kuridhishwa na utekelezaji wake.
Pamoja na kuona kasi  ya ujenzi huo  unavyoendelea  viongozi hao wamesisitiza ujenzi huo  uongezewe  kasi ili ukamilike kwa haraka.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi kata ya Kilimani Nathani Chibeye amesema ujenzi huo wa shule ya msingi utakuwa mkombozi kwa kata ya kilimani.
 "Kwa kuwa Kata hii tangu ipate Uhuru haijawahi kuwa na shule ya msingi jambo ambalo hupelekea watoto wa mitaa nne ya Kilimani kusoma katika shule za kata nyingine na kusababisha kutembea umbali mrefu kuitafuta elimu.,"Amesema
Licha ya hayo amesema wao  kama viongozi wa Chama Cha Mapinduzi kata ya Kilimani wanaishukuru Serikali ya awamu ya Sita chini  Rais Samia  Suluhu   Hassan kwa kuweza kuwapatia fedha za ujenzi wa shule hiyo ambayo itakuwa mkombozi kwa wananchi wa kata ya Kilimani.
Kwa upande wake Katibu wa Chama hicho Kata ya Kilimani Rotta Ndimbo ameitaka kamati ya ujenzi na mkandarasi kuhakikisha wanatanguliza uzalendo katika ujenzi wa shule hiyo ili thamani ya fedha zilizotengwa kwa ajili ya ujenzi huo zinatumika kama zilivyo kusudiwa.
Ziara hiyo ya viongozi wa Chama Cha Mapinduzi kata ya Kilimani ni mwendelezo wa kukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa na serikali katika kata ya Kilimani ili kuhakikisha utekelezaji wa ilani ya chama unafanikiwa.
 





 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 

 
 
 
 
 
 
 
 
 
No comments:
Post a Comment