Mradi wa maji wa Murusagamba siku 30 kukamilika - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, October 3, 2023

Mradi wa maji wa Murusagamba siku 30 kukamilika


Wizara ya Maji imetoa kiasi cha shilingi milioni 250 ili kuanza kutekeleza mradi wa maji katika kijiji cha Murusagamba, Ngara mkoani Kagera ambapo Mkuu wa wilaya ya Ngara Kanali Mathias Kahabi ameelekezwa kutumia nguvu kazi ya wafungwa kuchimba mitaro ukamilike katika siku 30 ili mradi uwe umekamilika na wananchi wakabidhiwe.

Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) amesema hayo akiwa katika ziara ya kikazi katika kata Murusagamba, wilayani Ngara kufuatia agizo alilopewa na Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Dotto Biteko (Mb) kufanyia kazi changamoto ya upatikanaji wa maji katika eneo hilo. 

Amesema kuongezeka kwa idadi ya watu katika kijiji cha Murusagamba kumesababisha huduma ya maji kutotosheleza hivyo mradi huo utawekewa miundombinu mipya ili maji yafike kwa wananchi.

Waziri Aweso amemuagiza Meneja wa Wakala wa Usambazaji Maji Vijijini (RUWASA) mkoa wa Kagera kutangaza mradi wa maji wa kijiji cha Ntanga wenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 700 ili wananchi wa kijiji hicho waanze kupata maji.


Pamoja na hayo, amemtaka mkandarasi anayetekeleza mradi wa maji wa Kumubuga kuripoti katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya kutoa maelezo ya lini atamaliza mradi anaotekeleza kutokana na kuchelewa kwa mradi huo.

No comments:

Post a Comment