MWENGE WA UHURU WAWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA MAJI NZUGUNI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, October 3, 2023

MWENGE WA UHURU WAWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA MAJI NZUGUNI


Na Selemani Kodima ,Dodoma

MWENGE wa Uhuru kitaifa 2023 umeweka jiwe la msingi katika mradi wa Maji wa Nzuguni jijini Dodoma ambao utaongeza hali ya uzalishaji wa maji katika jiji la Dodoma kutoka lita milioni 68.6 hadi lita milioni 76 sawa na ongezeko la Asilimia 11 kwa Siku.

Uweka wa Jiwe la Msingi la Mradi huo limefanywa leo na Mkimbiza Mwenge Kitaifa, Abdallah Shaibu Kaimu ambapo baada ya Mwenge kukagua Mradi huo amesema hatua ya mradi huo ni jitihada za serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassani .


Awali akisoma taarifa ya Mradi huo ,Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya maji safi na Usafi wa Mazingira DUWASA Mhandisi Aron Joseph amesema kuwa lengo la Mradi huo ni kuboresha huduma ya maji kwa kuongeza hali ya uzalishaji maji katika jiji la Dodoma.

Mhandisi Aron amesema hadi sasa Mradi huo umefika Asilimia 85 za Utekelezaji wake ambapo Mamlaka hiyo inatekeleza Mradi huo kupitia Wazabuni wa Saba .
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini na Waziri wa Madini Mhe,Anthony Mavunde amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa namna alivyoweza kuwatatulia changamoto ya Maji hasa katika kata ya Nzuguni.


Mradi huo mkubwa unaotekelezwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira (DUWASA) unagharimu Sh4.8 bilioni na unategemewa kuongeza asilimia 11 ya upatikanaji wa maji katika Jiji la Dodoma kwa kuwanufaisha wakazi 75,968.

Itakumbukwa kuwa Jiji la Dodoma linazalisha nusu ya mahitaji ya maji ambapo mahitaji ya maji ni lita milioni 133 kwa siku na yanayozalishwa ni lita milioni 67.8 hivyo kuwa na upungufu wa lita milioni 66.7 kwa siku.

No comments:

Post a Comment