PROF. KATUNDU ARIDHISHWA NA UJENZI WA MRADI WA MAJI NZUGUNI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, October 28, 2023

PROF. KATUNDU ARIDHISHWA NA UJENZI WA MRADI WA MAJI NZUGUNI


Na Mwandishi wetu - Dodoma

LEO Oktoba 28,2023 Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Prof. Jamal Katundu ametembelea na kukagua maendeleo ya Mradi wa maji Nzuguni na kuridhishwa na kazi inayoendelea.

Aidha amejionea maandalizi ya uchimbaji wa kisima kikubwa kitakachokuwa na urefu wa mita 300 kwenda chini kitakachochibwa eneo Nzuguni pamoja na visima vingine vya kawaida vinavyoendelea kuchimbwa katika eneo hilo.

Pia ametembelea kituo cha kuzalisha na kusukuma maji cha Mzakwe na kujionea jinsi shughuli za uzalishaji zinavyofanyika.


Prof. Katundu katika ziara hiyo ameilekeza DUWASA pamoja na Ofisi ya Bonde la Wami/Ruvu kuhakikisha wanapata vyanzo vingine vya maji haraka ili kupunguza au kuondoa kabisa changamoto ya maji katika jiji la Dodoma.

"Ninachotaka kuona Dodoma ambayo ni Makao Makuu inakuwa na maji ya kutosha, tafuteni vyanzo vingine chimbeni visima tumalize changamoto hii". amesema Prof. Katundu.

No comments:

Post a Comment