TIMU YA KAMBA, NETIBOLI TAMISEMI ZATINGA HATUA YA MTOANO - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, October 4, 2023

TIMU YA KAMBA, NETIBOLI TAMISEMI ZATINGA HATUA YA MTOANO


Na. Asila Twaha, Iringa

Timu ya wanawake ya kuvuta kamba na netiboli TAMISEMI zimeingia hatua ya mtoano baada ya kucheza mechi 4 na kushinda kupata nafasi nzuri kwa timu zote mbili kuingia hatua hiyo.

Mapema asubuhi Oktoba 3, 2023 katika viwanja vya Mkwawa Mkoani Iringa timu ya kamba ilicheza na wapinzani wake Wakili Mkuu na kuwashinda kwa pointi 2-0 huku timu ya netiboli kucheza katika uwanja wa Chuo Kikuu cha RUAHA kuwafunga wapinzani wao Ujenzi goli 29-21.

Kocha wa timu ya kamba TAMISEMI Chediel Masinga amesema pointi 7 walizoshinda kwa mechi nne walizocheza zimewapa nafasi kuingia katika hatua ya mtoano.

Amesema kwa hatua ya makundi timu ya TAMISEMI ilipangwa kundi F kucheza na RAS Kagera, Mashtaka, Mambo ya Nje na Wakili Mkuu na mechi zote hizo wamefanya vizuri.

Kwa upande wa timu ya netiboli kushinda na kufikia hatua ya mtoano walicheza na timu ya Mashtaka,TARURA,Ujenzi na Uchukuzi.

Michezo ya Shirikisho ya Wizara na Idara za Serikali yatafunguliwa tarehe 4 Oktoba, 2023

No comments:

Post a Comment