NA
K-VIS BLOG/KHALFAN SAID, MOROGORO
Mkurugenzi
wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi, kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw.
Richard Kayombo amesema uingizaji bidhaa kwa njia ya magendo sio tu kwamba
unapoteza mapato ya serikali bali pia ni hatari kwa afya za watumiaji.
Bw.
Kayombo ameyasema hayo wakati akijibu swali, nini madhara yanayotokana na
uingizwaji wa bidhaa za magendo nchini, kwenye kipindi cha maswali na
majadiliano katika Kongamano la Wakuu wa Vitengo vya Mawasiliano wa Taasisi za
Wizara ya Fedha na Wahariri wa Vyombo vya Habari, mjini Morogoro Oktoba 25,
2023.
“Kuna
madhara ya kukosa kodi, lakini uingizwaji wa bidhaa za magendo baadhi ni hatari
kwa afya za binadamu, zinaingizwa bila ya kupitia kwenye vyombo vya udhibiti
ubora.” Alisema.
Alitoa
mfano kule Wilayani Kilwa, Mkoa wa Lindi, ambako TRA, ilikamata sukari ikiwa
kwenye vifungashio vya viwanda vinavyotambulika nchini, lakini mazingira ya
eneo lililokuwa likitumika kufungashia sukari hiyo halikuwa zuri kiafya,”
alisema na kuongeza..pia tulikamata mafuta ya kula, kuna mengine tuliyamwaga
baada ya Mamlaka ya Udhibiti Ubora, kuthibitisha kuwa hayafai kwa matumizi ya
binadamu.” Alifafanua Bw. Kayombo.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, anayeshughulikia Huduma za Hazina, Bi. Jenifa Christian Omolo, akipena mikono na Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Richard Kayombo.Baadhi ya Washiriki wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi, wakati wa ufunguzi wa kongamano hilo.
Baadhi ya Washiriki wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi, wakati wa ufunguzi wa kongamano hilo.
Bi. Scola Malinga, kutoka Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha
No comments:
Post a Comment