NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID, MOROGORO
KAMISHNA
Msaidizi idara ya ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP), Wizara ya
Fedha, Bw. Bashiru Taratibu, amesema, mabadiliko ya sheria ya ubia kati ya
serikali na sekta binafsi yamelenga kumlinda mwekezaji.
Amesma
hayo wakati akiwasilisha mada ya Sheria ya PPP, mwishoni mwa kongamano la siku
mbili la wasimamizi wa mitandao ya kijamii (Online Media) na Wizara ya Fedha mjini
Morogoro, Oktoba 24, 2023.
Amesema
huko nyuma sheria haikuwa rafiki kuwezesha utekelezaji wa miradi kwa njia ya
ubia PPP.
“Ni
matarajio ya serrikali, kuwa baada ya marekebisho ya sheria ya PPP Sura ya 103
ya mwaka 2023 kuidhinishwa na Rais, ile miradi ya PPP zaidi ya 60, ambayo
imeandaliwa na pande zote mbili serikali na sekta binafsi, sasa itakwenda
kutekelezeka kwa manufaa ya pande zote.” Alisema.
Alisema
kabla ya sheria, moja ya vikwazo ilikuwa ni mamlaka za serikali, ambapo
walichukua hadi mwaka mzima kujadiliana kabla ya kufikia uamuzi, lakini
mabadiliko ya sheria hii yanaelekeza kuwa kila baada ya miezi mitatu itolewe
taarifa ya hatua iliyofikiwa ili uamuzi ufikiwe.
“Sheria
ya sasa inatamka ununuzi wa mbia ufanyike kwa uwazi na ushindani ili kumpata
mtu sahihi kwa kuzingatia vigezo vilivyowekwa.” Alisisitiza Bw. Taratibu na
kuongeza..
“Tunaenda
kwenye sekta binafsi ili kupata vitu vitatu ambavyo ni pamoja na kupata fedha
ya kutekeleza mradi, ujuzi wa uendeshaji ambao serikali haina, pia teknolojia.”
Alifafanua.
Aidha,
Sheria hii ya sasa inatamka kuwa Mbia lazima awe amesajili kampuni yake kwa
mujibu wa sheria ya makampuni ya Tanzania.
Alisema
baadhi ya miradi ya PPP ambayo ‘imeiva’ ni pamoja na mradi wa ujenzi wa
barabara ya njia nne kila upande, Kibaha-Chalinze awamu ya kwanza na Chalinze- Morogoro.
KAMISHNA Msaidizi idara ya ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP), Wizara ya Fedha, Bw. Bashiru Taratibu
Mwenyekiti
wa washiriki, Bw. Mathias Canal, akizungumza wakati wa kufunga kongamano hilo
Kamishna
Msaidizi idara ya ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP), Wizara ya
Fedha, Bw. Bashiru Taratibu (katikati) akijadiliana jambo na Mkuu wa Kitengo
cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha, Bw. Benny Mwaipaja (kulia) na
Afisa Tawala Wizara ya Fedha, Bw. Bw. Brighton Ngowo
Baadhi
ya washiriki
Mhasibu Mwandamizi kutoka Ofisi ya Mhasibu Mkuu wa Serikali, Wizara ya Fedha, CPA. Jenipha J. Ntangeki
Mhariri
wa Maudhui Mtandaoni, kutoka Mwananchi Communications, Bw. Muyonga Jumanne
(kushoto) akichangia wakati wa majadiliano. Kulia ni Mmiliki wa Okuly Blog, Bw.
Okuly Julius.
No comments:
Post a Comment