WAZIRI BASHUNGWA AONGOZA HARAMBEE UJENZI WA KANISA BARIADI. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Sunday, October 8, 2023

WAZIRI BASHUNGWA AONGOZA HARAMBEE UJENZI WA KANISA BARIADI.


Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa, ameshiriki Misa Takatifu na kuongoza harambee ya kuchangia Ujenzi wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Luka Jimbo la Bariadi Mkoani Simiyu, Leo tarehe 08 Oktoba 2023.

Waziri Bashungwa akitoa taarifa baada ya harambee hiyo amesema kiasi kilichopatikana ni Milioni 28.8 ambapo ni pesa taslimu na ahadi.

Aidha, Waziri Bashungwa ametoa wito kwa waamini walioshiriki Misa hiyo kuendelea kuchapa kazi na kuunga mkono Seriikali inayoongozwa na Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Waziri Bashungwa ameshiri Misa hiyo katika mwendelezo wa ziara ya kikazi katika Mikoa ya Mbeya, Iringa, Singinda, Simiyu na ataendelea katika Mkoa Mara, Mwanza na Kagera.

No comments:

Post a Comment