waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amezuru Kaburi la Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na kutembelea Makumbusho yake katika kijiji cha Mwitongo, Wilayani Butiama Mkoani Mara. Leo tarehe 08 Oktoba 2023.
Waziri Bashungwa amepata nafasi ya kuongoza dua ya kumuombea Baba wa Taifa, Kuwasha mshumaa pamoja na kuweka mashanda ya Maua katika kaburi la Baba wa Taifa.
Pamoja na mambo mengine amepata nafasi ya kutembelea maeneo mbalimbali ya kumbukumbu katika Makazi ya Baba wa Taifa katika kijiji cha Mwitongo.
Waziri Bashungwa anaendelea na ziara ya kikazi katika Mikoa ya Mbeya, Iringa, Singida, Simiyu na sasa yupo Mkoa Mara ambapo atatembelea na kukagua miradi na shughuli mbalimbali zianzoendelea katika Sekta ya Ujenzi.
No comments:
Post a Comment