Na Okuly Julius - Dodoma
Dkt.Biteko ameyasema hayo leo Novemba 8,2023 jijini Dodoma,wakati akifungua Kikao Cha Baraza la Wafanyakazi wa Mamlaka hiyo ambapo amewasisitiza pia wafanyakazi wa EWURA kuwajibika ipasavyo katika kutekeleza majukumu yao kwa kuhakikisha kuwa watoa huduma wanafanya ushindani wenye tija na ufanisi wa kiuchumi,kulinda maslahi ya walaji na mitaji ya Watoa Huduma pamoja na kuhakikisha upatikanaji wa huduma kwa makundi yote ikiwemo ya watu wanaoishi vijijini.
“Gharama za uagizaji wa mafuta zilikuwa kubwa mno na hapakuwa na sababu kubwa zozote zilizokuwa zinafanya gharama hizo kuwa kubwa ndio maana niliwapa maelekezo wakazitizame upya na nimeshukuru sana kwa sababu mmetumia muda mfupi sana kuzipitia na gharama zimeshuka na kupunguza makali kwa watumiaji,”amsema Dkt.Biteko
Pia Dkt.Biteko ameitaka Mamlaka hiyo kuzingatia Maslahi ya Watanzania na maslahi ya nchi katika kazi zake za Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji ili Watanzania wapate huduma bora na kwa unafuu mkubwa.
“Tambueni kuwa Taifa lina wategemea sana ,hivyo fanyeni kazi zenu kwa weledi na ubunifu mkubwa unaoendana na kasi ya teknolojia na maendeleo ya dunia kanuni na miongozo yenu mnayotumia katika utekelezaji wa majukumu iundwe katika mifumo rafiki kulingana na hali iliyopo ili ilenge kuleta matokeo chanya kwa ustawi wa Taifa na hivyo Watamzania waendelee kupata huduma bora na kwa gharama stahiki ,“amesema Dkt.Biteko
Naye Mkurugenzi Mkuu wa EWURA Dkt. James Andilile amesema kuwa uwepo wa Baraza hilo la wafanyakazi wa EWURA imekuwa kichochoe kikubwa cha maendeleo kutokana na ushirikiano wao katika mambo mbalimbali ikiwemo ushauri na maoni mbalimbali hasa katika bajeti ya kila mwaka ili kuweza kuboresha utendaji.
“EWURA inategemea sana uwepo wa baraza la wafanyakazi kwani wamekuwa ni watu muhimu sana ambao wametusaidia kutengeneza maono ya kuboresha utendaji hasa wa Menejimenti na watumishi mahali pa kazi,”amesema Andilile
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu TUGHE taifa Bw. Rugemalila Rutatinwa amesema kuwa ,Baraza la EWURA ni kati ya Mabaraza yanayojitahidi sana kutatua changamoto zinazowakabili Wafanyakazi na wanashirikiana vyema na Chama cha wafanyakazi na Muajiri ili kuhakikisha kunakuwa na utulivu mahala pa kazi.
No comments:
Post a Comment