KAMPENI YA "TUMEWASIKIA TUMEWAFIKIA" YAZINDULIWA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, November 1, 2023

KAMPENI YA "TUMEWASIKIA TUMEWAFIKIA" YAZINDULIWA

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Nnauye, akizungumza Leo Novemba 1,2023 Jijini Dodoma, wakati akizindua mikutano ya wakuu wa mikoa, wakurugenzi na vyombo vya habari, ambapo amesema pamoja na kazi kubwa inayofanywa na serikali ya awamu ya sita wananchi bado hawana taarifa za kutosha.
Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo) Mobhare Matinyi,akizungumza Leo Novemba 1,2023 Jijini Dodoma, wakati wa uzinduzi wa mikutano ya wakuu wa mikoa, wakurugenzi na vyombo vya habari.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule,akizungumza Leo Novemba 1,2023 Jijini Dodoma, wakati wa uzinduzi wa mikutano ya wakuu wa mikoa, wakurugenzi na vyombo vya habari.

Na Okuly Julius-Dodoma

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Nnauye, ametoa wito kwa wakuu wa mikoa na wakurugenzi wa Halmashauri zote Nchini kuhakikisha wanatoa ushirikiano kwa Idara ya habari MAELEZO na waandishi wa habari ili kupata maudhui mazuri yatakayotumika katika vyombo vya habari kutangaza mafanikio ya Serikali kwa Wananchi.

Mhe. Nape Nnauye ameyasema hayo Leo Novemba 1,2023 Jijini Dodoma, wakati akizindua mikutano ya wakuu wa mikoa, wakurugenzi na vyombo vya habari, ambapo amesema pamoja na kazi kubwa inayofanywa na serikali ya awamu ya sita wananchi bado hawana taarifa za kutosha.

Amesema Kampeni ya Tumewasikia Tumewafikia inawataka wakuu wa mikoa yote 26 na wakurugenzi wa halmashauri zote 184 nchini, kuandaa mikutano na vyombo vya habari ili kutangaza kwa wananchi kazi zinazofanywa na serikali yao.

Nnauye, amesema anaipongeza Idara ya Habari (Maelezo) kwa kuja na ubunifu huo na kuja kampeni hiyo ambayo wakuu wa mikoa pamoja na wakurugenzi wa halmashauri nchini wataitumia kuandaa mikutano na vyombo vya habari.

“Programu hii ya Tumekusikia Tumekufikia, itakwenda nchi nzima ambayo lengo lake ni kufahamisha umma kazi kubwa iliyofanywa na inayoendelea kufanywa na serikali ya awamu sita kwenye sekta za maji, afya, miuondombinu na miradi mingine ya maendeleo nchini”alisema

Kadhalika, alisema lengo jingine la kampeni hiyo ni kuongeza chachu ya mawasiliano kati ya wananchi na serikali yao kwa kuwa itatoa nafasi ya wakuu wa mikoa pamoja na wakurugenzi kueleza mambo ambayo yamefanywa.

“Serikali inatoa fedha nyingi za utekelezaji wa miradi mbalimbali hivyo wananchi wanayo haja ya kufahamu kodi zao zinafanya nini tunapozungumzia, maji, afya lazima wananchi wafahamu nini kinaendelea,

Na kuongeza kuwa “Tumekuwa na utaratibu wa kufanya mikutano hii katika ngazi za wizara na taasisi hivyo mikutano hii itasaidia wananchi wa ngazi ya chini kabisa kufahamu nini serikali yao inafanya na huko ndiko pia serikali imekuwa ikipeleka kiasi kikubwa cha fedha katika utelezaji wa miradi mbalimbali”alisema Nnauye

Amesema pia kupitia program hiyo wananchi watapata fursa ya kueleza kile ambacho serikali yao imefanya na kimewanufaisha kwa namna gani.

Kwa upande wake Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo) Mobhare Matinyi, amesema lengo la kuanzishwa kwa kampeni hiyo ni kuwafikishia wananchi ngazi ya chini taarifa kuhusu kazi inayofanywa na serikali yao.

“Hivi sasa serikali inafanya mambo makubwa sana katika maeneo mbalimbali lakini ukiangalia ukubwa wa kazi unaofanywa na taarifa zinavyosemwa ni mbigu na ardhi.

“Hivyo kampeni hii itasaidia kufikisha taarifa sahihi kwa wananchi kuhusu kile kinachofanywa na serikali yao na kuondoa ‘gap’ lililopo hivi sasa baina ya serikali na wananchi wake”amesema Matinyi

Hata hivyo, alisema kampeni hiyo baada ya kuzinduliwa jijini Dodoma itakwenda katika mikoa yote na halmashauri zake zote 184 nchini ambapo awamu ya kwanza itakuwa ni mikoa ya Dodoma, Morogoro, Pwani na Dar es Saalam.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule amesema kuwa Serikali imetoka zaidi ya Shilingi bilioni 81 Kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya sekta ya Elimu katika mkoa wa Dodoma ambapo imejenga Madarasa mapya zaidi ya 1400 na Shule mpya kabisa 124 na kupelekea ongezeko la wanafunzi wanaojiunga na kidato Cha kwanza na Tano kuongezeka.

"Serikali ya Awamu ya Sita Chini ya Dkt.Samia imeufanyia mambo makubwa mkoa wa Dodoma kuanzia sekta ya afya,Elimu, barabara na maeneo mengine hivyo ndani ya miaka hii mitatu mkoa wa Dodoma unaendelea Kwa Kasi katika sekta zote tnamshukuru sana," amesema Senyamule 


No comments:

Post a Comment