MTUMISHI WA MLOGANZILA AZINDUA KITABU KINACHOHUSU AFYA YA AKILI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, November 15, 2023

MTUMISHI WA MLOGANZILA AZINDUA KITABU KINACHOHUSU AFYA YA AKILI


Wataalamu wa afya wametakiwa kujikita zaidi katika kufanya tafiti juu ya mambo yanayoikumba jamii na kuweka maarifa hayo katika maandishi ili kuisaidia katika kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii.

Rai hiyo imetolewa leo na Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Tiba Hospitali ya Taifa Muhimbili Mloganzila Dkt. Faraja Chiwanga, akizungumza kwa niaba Mkurugenzi Mtendaji , wakati akizindua kitabu kilichoandikwa na mtumishi wa MNH- Mloganzila kinachoitwa “Afya ya Akili ni kipaumbele chako, tuongeze ufahamu”.


Dkt. Chiwanga amesema kuwa tatizo la afya ya akili ni kubwa sana na limeshika kasi ulimwenguni hivyo ni wakati sasa wa wataalamu wa afya kukuza uelewa kwa jamii ili kuwasaidia kukabiliana na changamoto hizo.

“Tunaishi katika ulimwengu unaobadilika haraka na mazingira yetu yamejaa changamoto zinazoleta msongo wa mawazo, hivyo huu niwakati wa taasisi za afya kushirikiana na wataalamu wa afya ya akili pamoja na jamii kwa ujumla ili kukabiliana na matatizo ya afya ya akili” amesema Dkt. Chiwanga.

Kwa Upande wake mwandishi wa kitabu hicho Bi. Consolatha Asenga amesema kuwa lengo la kuandika kitabu ni kuisaidia jamii kupata uelewa juu ya kuilinda afya ya akili na kuwasaidia wengine ambao tayari wameingia kwenye changamoto hiyo.

“Katika kitabu changu kinachoitwa (Afya ya akili ni kipaumbele chako, tuongeze ufahamu) nimezungumzia maswala mbalimbali yanayoikabili jamii na namna gani jamii inaweza kukabiliana na matatizo hayo ili kuilinda afya ya akili” Amesema Dkt. Bi. Consolatha

Ameongeza kuwa kitabu hicho kinatoa muongozo kuhusu hatua za kuchukua ili kukabiliana na mitazamo hasi iliyojengeka katika jamii kuhusu suala la afya ya akili na changamoto zake.

No comments:

Post a Comment