Mzozo wa israel na Hamas:Hakuna suluhisho la kijeshi au la usalama - Mfalme Abdullah wa Jordan - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, November 14, 2023

Mzozo wa israel na Hamas:Hakuna suluhisho la kijeshi au la usalama - Mfalme Abdullah wa Jordan


CHANZO NI BBC SWAHILI


Mfalme Abdullah wa Jordan amekataa mpango wowote wa Israel wa kukalia sehemu za Gaza au kuunda maeneo ya usalama ndani ya eneo hilo.


Mwanamfalme huyo aliwaambia wanasiasa wakuu katika kasri ya kifalme kwamba hakuwezi kuwa na "suluhisho la kijeshi au la kiusalama" kwa mzozo kati ya Israel na Wapalestina, vyombo vya habari vya serikali viliripoti.


Amenukuliwa akisema kuwa chanzo kikuu cha mgogoro huo ni kuwanyima Wapalestina "haki halali" za Wapalestina.


"Suluhu huanzia hapo na njia nyingine zozote zitashindwa na vurugu na uharibifu vitaendelea," alisema pia.


Waziri Mkuu wa Israel Benjamini Netanyahu kuwa Israel itakuwa na "jukumu la jumla la usalama" kwa Ukanda wa Gaza "kwa muda usiojulikana" wakati wa mahojiano wiki iliyopita.


Jordan imepokea idadi kubwa ya wakimbizi wa Kipalestina.

No comments:

Post a Comment