"SIKILIZENI NA MTATUE KERO ZA WANANCHI” SENYAMULE - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, November 20, 2023

"SIKILIZENI NA MTATUE KERO ZA WANANCHI” SENYAMULE


Na. Asila Twaha, OR – TAMISEMI

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mheshimiwa Rosemary Senyamule amewataka Watendaji wa Kata na Maafisa Tarafa wa Mkoa wa Dodoma kuwasikiliza na kutatua kero za wananchi kwa kuwa wao ndio kiungo cha Serikali waliopewa dhamana ya kuonana na wananchi moja moja.


Mheshimiwa Senyamule ametoa kauli hiyo wakati akifungua mafunzo ya kuwajengea uwezo Watendaji wa Kata na Maafisa Taarafa wa Halmashauri yaliyoandaliwa na Ofisi ya Rais -TAMISEMI yaliyofanyika Jijini Dodoma leo Novemba 20, 2023.


Amesema, lengo la mafunzo hayo ni kuwaongezea ujuzi na maarifa katika kutekeleza majukumu yao ili kupunguza na kuwaondolea kabisa changamoto katika kuwahudumia wananchi na wadau mbalimbali wa maendeleo kwa kurahisisha na kuimarisha mahusiano mazuri kati ya Serikali na wananchi.


“Utekelezaji na utendaji mzuri wa majukumu yenu katika kusikiliza na kutatua kero za wananchi inaisaidia moja kwa moja Halmashauri kufikia malengo yake katika kutekeleza malengo ya sekta mbalimbali” Mhe. Senyamule


Alikadhalika ameeleza uwepo wa baadhi ya Watendaji wa Kata na Maafisa Tarafa wasiowajibika ipasavyo katika majukumu yao, hali inayosababisha malalamiko kutoka kwa wananchi wakidai kutosikilizwa kwa kero zao.


“Mmewekwa pale kwa ajili ya kuwahudumia wananchi, wapeni nafasi na heshima wananchi ili waipende nchi yao”. Alisistiza Mhe. Senyamule



Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Serikali za Mitaa, Ofisi ya Rais – TAMISEMI Bi. Angelista Kihaga, amesema mafunzo hayo ya siku mbili yatawashirikisha walengwa hao katika mada mbalimbali ikiwa ni pamoja na Muundo na majukumu ya kada na matarajio ya Serikali na wananchi wanaowahudumia Pamoja na ushughulikiaji wa kero za wananch.


Awali akitoa mada katika mafunzo hayo Mhadhiri kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo Paulo Fati, ametoa wito kwa Maafisa hao kuleta faraja kwa wananchi wanaowahudumia na sio kuwa kilio kwa wanaowaongoza akisisitiza misingi ya kiongozi bora kuwa ni yule anaeona changamoto na kuzifanya kuwa fursa.


Mafunzo hayo kwa Watendaji wa Kata na Maafisa Tarafa ni muendelezo wa mafunzo yanayofanyika nchi nzima kwa nyakati tofauti chini ya uratibu wa Ofisi ya Rais -TAMISEMI kwa kushirikiana na Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo na Chuo cha Utumishi wa Umma yakilenga kuwakumbusha miiko na maadili ya utumishi wa umma.

No comments:

Post a Comment