Ashrack Miraji , Same Kilimanjaro
Mbunge wa Same Magharibi DKT David Mathayo amesema Michezo inawajenga vijana kuwa na mahusiano mazuri Katika nyanja mbali mbali na kuweza kutimiza ndoto zao pia kuachana na vitendo viovu kama ukabaji na kutumia madawa ya kulevya, bangi na mirungi
Hayo ameyasema wakati akifanya mahojiano na Mwandishi wetu kuelekea uzinduzi wa Dtk Mathayo Cup tarehe 26 Novemba Katika jimbo la Same Magharibi mkoani Kilimanjaro ambazo Timu 56 zinatarajiwa kushiriki mashindo hayo
"Dhamira yangu kwa vijana ni kubwa mno ni kutaka kuona wanafika mbali na kutimiza ndoto zao hivyo nitakuwa nao bega kwa bega katika kuleta maendeleo chanja kwenye jimbo letu la Same Magharibi kuhakikisha nakuza vipaji vyao," amesema Dkt Mathayo
Mhe Mathayo amesema pia Mathayo Cup hiyo ni jitiada za kumuunga Mkono Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika sekta ya Michezo.
"tumeona Rais akifatilia Michezo tofauti kwa ukaribu Sana pia na kuzipa Timu zetu hamasa Katika mashindano ya kimataifa na Mimi kama muwakilishi wake Katika jimbo la Same Magharibi nitahakikisha vijana wa Same Magharibi wananufaika jatika Michezo na Shughuli Mbalimbali za kiuchumi,
Na kuongeza kuwa" niseme Ukweli wa dhati Mhe Rais Dkt. Samiha amenifanyia makubwa Katika jimbo langu amenijengea vituo vya Afya ,Barabara,shule namshukur sana kwa mchango wake mkubwa hasa kwa Wananchi wangu wa jimbo la Same Magharibi,"ameeleza Dkt.Mathayo
No comments:
Post a Comment