PAROKIA YA KIWANJA CHA NDEGE YAWAKUMBUKA WAATHIRIKA HANANG' - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Sunday, December 17, 2023

PAROKIA YA KIWANJA CHA NDEGE YAWAKUMBUKA WAATHIRIKA HANANG'

Waziri wa Nchi Ofisi ya waziri Mkuu, (Sera Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama akipokea hundi ya shilingi milioni 5 kutoka kwa Kamati ya Caritas Parokia ya Mwenyeheri Maria Theresa Ledochowaska Kiwanja Cha ndege Dodoma.

NA. MWANDISHI WETU

Padre Emmanuel Mtambo wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mwenyeheri Maria Theresa Ledochowaska amesema Kanisa linawajibu wa kuchangia watanzania wenzetu waliopata janga la mafuriko ya Mawe na Matope kutoka Mlima Hanang’.

Alisema Parokia ya Mwenyeheri Maria Theresa Ledochowaska Kiwanja cha Ndege kupitia kamati ya Caritas ambayo inashughulikia wanaohitaji, leo tarehe 17/12/2023 jijini Dodoma imetoa hundi ya shilingi milioni 5 ikiwa ni sehemu ya kushirikiana na serikali kusaidia waathirika.

“Kama Parokia na Kanisa; tunapaswa kufanya sehemu yetu, kupitia michango yetu tunayotoa katika akaunti ya Caritas” alifafanua

Mchango huo umepokelewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya waziri Mkuu, (Sera Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama.

No comments:

Post a Comment