NDEJEMBI AAGIZA TAKUKURU KUCHUNGUZA UJENZI WA SHULE YA JAJE - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Sunday, December 17, 2023

NDEJEMBI AAGIZA TAKUKURU KUCHUNGUZA UJENZI WA SHULE YA JAJE


OR-TAMISEMI


NAIBU Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe. Deogratius Ndejembi amewasimamisha kazi wahandisi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga, Issa Mchezo na Mussa Mkonachi kutokana na usimamizi mbovu wa miradi huku akiagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kuchunguza manunuzi katika ujenzibwa Shule ya Msingi Jaje.

Mhe Ndejembi ametoa agizo hilo jijini Tanga katika ziara yake ya kukagua miradi ya ujenzi wa Shule mpya ya Msingi Jaje iliyojengwa kupitia mradi wa BOOST na Shule ya Sekondari Magaoni iliyojengwa kwa fedha za mradi wa SEQUIP.

“Serikali hii ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan haitamvumilia mtumishi yeyote ambaye atashindwa kusimamia miradi kwa uadilifu. Tutachukua hatua kwa watendaji watakaocheza na fedha za miradi ikiwa ni pamoja na kuka na fedha bila kutumika na kuchelewasha ukamilikaji wa miradi. Hivyo mhandisi wa hapa umeonesha udhaifu huo na hivyo namuagiza nakusimamisha kazi kwa uzembe huo."

“ TAKUKURU niwatake mlete timu yenu mara moja ya uchunguzi ili mchunguze manunuzi kwenye miradi hii. Haiwezekani Jiji la Tanga saruji iuzwe bei ya juu zaidi ya Pangani. Chunguzeni na ripoti yenu tuipate lakini pia mchukue hatua za kisheria,” amesema Mhe. Ndejembi.

Katika ziara yake jijini humo Naibu Waziri Ndejembi pia ametembelea mradi wa soko la machinga Kange na kuzungumza na watumishi wa halmashauri ambapo amewataka kuacha kufanya kazi kwa mazoea na wawatumikie wananchi ili kutekeleza dhana ya Rais Samia ya kuhakikisha watanzania wanapata huduma iliyo bora.

No comments:

Post a Comment