Na Okuly Julius - Dodoma
Waziri wa
Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Balozi
Pindi Chana ametoa wito kwa taasisi na vyombo vya Serikali, mashirika
ya kiraia,ya wanawake, vijana, sekta binafsi, vyombo vya habari, na mfumo wa Umoja
wa Mataifa kuungana ili kukabiliana na ukatili dhidi ya wanawake na wasichana
kwa wigo wa kimataifa.
Balozi Chana
ametoa wito huo leo Disemba 6,2023 jijini Dodoma, wakati akizindua muendelezo wa shughuli ya
Maadhimisho ya Siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia mkoa wa Dodoma.
Akitoa wito
huo,Balozi Chana amewaomba wadau wa
Maendeleo kuongeza juhudi za pamoja kuzuia ya ukatili kwa wanawake na wasichana
‘‘ Niwaombe
muongeze mashirikiano ya muda mrefu na
usaidizi kwa kuunga mkono juhudi za Serikali
kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia miongoni mwa jamii,’’ alisisita
waziri Chana.
Sambamba na
hilo akawakumbusha wadau wa maswala ya jinsia kushiriki mapambano hayo hasa kwa
watu wasiofikiwa .
“Kwa
mashirika yanayotetea haki za wanawake na Watoto, niwaombe tujikite zaidi
katika maeneo ya pembezoni kwani kule ndipo kwenye changamoto zaidi. Na hii
inatokana na ukweli kwamba, elimu ya masuala haya bado haijafika vya kutosha
kwahiyo jamii bado inaamini katika mila na desturi,’’ aliongeza waziri huyo
Aidha atumia
fulsa hiyo kuwakumbusha watendajiwa
serikali kuendelea kutoa ushirikiano kwa wadau wote kwenye mapambano hayo.
“niwasihi
muendelee kushirikiana na Serikali katika utekelezaji wa Mama Samia Legal Aid
Campaign ikiwa ni mojawapo ya mkakati madhubuti wa kuelimisha jamii kuhusu
kuzuia na kukabiliana na ukatili wa kijinsia hapa nchini hususan kwa wanawake
na watoto,”alikumbusha Balozi Chana
Sambamaba na
hilo, amezitaka Taasisi za umma, kuendelea kuwajengea uwezo wanawake na wasichana
kwa kuwashirikisha kwenye nafasi mbalimbali za siasa, utungaji sera, na uamuzi
kutoka ngazi kijiji au mitaa, taifa za
kimataifa.
Kwa upande
wa wananchi amewakumbusha kushirikiana na viongozi wa Serikali za mitaa na Serikali Kuu,
kuimarisha ulinzi ili kuzuia na kuondoa tabia za ukatili, unyanyasaji, vitisho na ubaguzi dhidi ya
wanawake, watoto na watetezi wa haki za binadamu.
Kwa upande
wa vyuo vya taalamu Waziri huyo amewataka
kutumia vyema dhamana waliyopewa katika utekelezaji
wa majukumu yao kwa kuzingatia maadili ya kazi ,kwa kupiga vita rushwa au upendeleo unaosababisha ukatili wa
kinjisia kwa wanawake na wasichana
wawapo chuoni.
Akizungumza kwa niaba ya Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) Prof.Albino Tenge amesema kuwa chuo hicho kinaendelea kuwajenga vijana katika misingi ya kuwa mabalozi wema wa kupamabana na masuala ya ukatili wa kijinsia na kuwapa nafasi ya kushiriki kampeni mbalimbali ikiwa ni kwa njia ya kwenda kutoa elimu kwa jamii au kushiriki midahalo mbalimbali Sio tu katika siku hizi 16.
“Tunaweza tu
kusonga mbele na kuushinda Ukatili wa Kijinsia ikiwa tutazungumza na kupaza
sauti. Hivyo sisi Chuo Kikuu Cha Dodoma
kwa pamoja wote tunasema, Unyanyasaji wa kijinsia hauna nafasi katika nchi hii.
Sio tu katika siku hizi 16, bali iwe katika maisha yetu ya kila siku. Kila
mmoja wetu ajitathimini ni kwa kiasi gani anachangia kuzuia vitendo vya ukatili
wa kijinsia katika familia yake, eneo lake la kazi na jamii kwa ujumla, Na
kisha achukue hatua,”amesema Prof. Tenge.
Hadi sasa
jumla ya madawati 1,850 ya jinsia yameanzishwa kati ya hayo 1,128 kwenye shule
za msingi na 772 shule za Sekondari.
Kwa upande wa Taasisi za elimu za juu hadi sasa jumla ya madawati 273 yameanzishwa likiwemo dawati la Chuo Kikuu cha Dodoma na kufanya idadi hiyo kufikia asilimia 44 ya lengo la kuwa na madawati 612 ifikapo mwezi Juni 2024.
No comments:
Post a Comment