Mhe Dkt Nchemba ametoa pole kwa Wananchi wote waliokumbana na athari za maporomoko ya Ardhi yaliyoambatana na Mvua na kusababisha vifo vya watu 89 na wengine 100 kuumia.
Dkt Nchemba, akizungumza na viongozi wa wilaya hiyo alisema Serikali imeendelea kutoa huduma na misaada mbalimbali kwa waathirika wa tukio hilo huku akiahidi kuwa jitihada za kusaidia wananchi zitaendelea kwa uharaka kulingana na mahitaji ya walengwa ikiwemo ujenzi wa Miundombinu ya maji, soko, barabara n.k
"Kama alivyoelekeza Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kusaidia wananchi wetu lazima tutafanya jitihada zote wenzetu wapunguze uchungu wa kile kilichotokea" alisema Dkt. Nchemba
"Tuendelee kuchukua tahadhari kwa sababu hatujui kama hali ya hewa inaweza kubadilika muda wowote ambao hatuujui kama ilivyotokea hii hakuna aliyekuwa akijua lakini niwapongeze wataalamu wote, Mawaziri kwa namna ambavyo mmekuwa mkisaidia wananchi wetu hapa Hanang" aliongeza Dkt. Nchemba.
No comments:
Post a Comment