UDOM YAPANDA MITI KUELEKEA MAADHIMISHO YA MIAKA 60 YA MUUNGANO WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, January 27, 2024

UDOM YAPANDA MITI KUELEKEA MAADHIMISHO YA MIAKA 60 YA MUUNGANO WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR


Na Carlos Claudio , DODOMA 

Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Mhe. Dkt Khamis Mkanachi amesisitiza viongozi kutunza miti inayopandwa ili kuepuka takwimu ya upandaji wa miti mingi ambayo haitaleta manufaa chanya katika taifa.

Dkt. Mkanachi ameyasisitiza hayo wakati akiendeleza zoezi la upandaji miti kuelekea Maadhimisho ya Miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, lililofanyika katika Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) leo Januari 27, 2024, lililoambatana na upandaji wa miti katika eneo la chuo.


“Tumekuwa na mtihani, miti ndio tunapanda lakini mikakati ya utunzaji hatuna, kwaio miti mingi haiwezi kuwa hai na kwa takwimu itaonekana kweli tumepanda miti mingi lakini ukija kwenye uhalisia hauioni miti hiyo kwaio mtendaji wa kata, viongozi wangu wa chama mliopo hapa jambo hili ni la kwenu, tunashukuru vijana wa Chuo Kikuu Cha Dodoma kwa zoezi la kushiriki nasi kwa maana ya kupanda lakini ilikja kwenye swala la kutunza na kuisimamia viongozi wa Chama, viongozi wa Kata, viongozi wa mtaa naomba jambo hili mkalichukue na liwe la kwenu".


“Ilani ya Chama Cha Mapinduzi ambacho ndio ulikuwa mkataba kati ya Chama Cha Mapinduzi na wananchi 2020/2025 inazungumzia zoezi la Ukijanishaji ya upandaji wa miti na kwa Dodoma ilani imetamka miti milioni 40 inatakiwa ipande na kwa maelekezo ya viongozi tuliyasikia kila halmashauri ipande miti milioni 1 na laki 5 kama ingekuwa ni agizo hilo peke yake kwa Dodoma kati ya wilaya 7 tulizonazo maana yake tungepanda miti takribani milioni 11 au milioni 12”.amesema Mhe. Mkalachi.

Amesema ni miti inapandwa kwa juhudi kubwa lakini kumekuwa hakuna mikakati ya kuitunza na miti mingi huishia kukosa matunzo na kufa.

Kwa upande wa makamu mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dodoma Prof. Lughano Kusiluka amehimiza wanafunzi wa chuo pamoja na wananchi wa Dodoma kutunza mazingira hasa rasilimali za miti kwani ni sehemu ya vivutio na chanzo cha mvua ya kutosha.

“Waliokaa Dodoma miaka mingi wanajua kwamba huko nyuma hakukuwa na upungufu wa mvua kiasi hiki, hakukuwa na mapungufu ya miti kiasi hiki lakini kwasababu ya kutotumia vizuri rasilimali za miti, kukata miti hovyo kwaajili ya mkaa na shughuli nyengine ambazo sio nzuri tumeishia sasa kuwa na hali ambayo sio nzuri na tunaanza kupungukiwa na maji tunapungukiwa na majani pia mvua inapungua kwaio sisi hapa Chuo Kikuu Cha Dodoma tumeitikia vizuri ajenda hii na mwaka jana tumepanda jumla ya miti elfu 20 lengo letu ni kuhakikisha kwamba tunakuwa sehemu ya mpango mikakati ya mpango kabambe wa kitaifa wa kuhifadhi na kusimamia mazingira ambayo ni programu ya miaka 10 iliyoanza 2022 ikielekea 2032 lakini itaendelea kuwepo kwakuwa Tanzania ipo milele.”amesema profesa Kusiluka.

Sambamba na hayo Profesa Kusiluka amewahimiza wanafunzi pamoja na wananchi waizungukao UDOM kutunza mioto kwani ni maisha ya baadae ikiwemo maji pamoja na changamoto za tabia ya nchi.



No comments:

Post a Comment