KAMATI YA BUNGE YA PIC YAIPONGEZA DUWASA UTEKELEZAJI MRADI WA MAJI NZUGUNI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Sunday, January 28, 2024

KAMATI YA BUNGE YA PIC YAIPONGEZA DUWASA UTEKELEZAJI MRADI WA MAJI NZUGUNI


Na Okuly Julius-Dodoma

KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma (PIC) leo Januari 28 jijini Dodoma imetembelea Mradi wa maji unaondelea katika eneo la nzuguni jijini Dodoma wenye thamani ya bilioni 4.4 na kujionea mradi ulipofikia kwa sasa ni asilimia 96.

Deus Sangu ambae ni mwenyekiti wa kamati hiyo na Mbunge wa Kwela akizungumza mara baada ya kutembelea mradi huo ametoa pongezi kwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa namna anavyoendelea kutoa fedha kwa ajili ya kuboresha upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama kwa wananchi.

Kamati hiyo imekagua ujenzi wa visima vitano vya maji katika kata ya Nzuguni,ambapo imesema mradi huo ukikamilika utaongeza hali ya upatikanaji wa maji katika jiji la Dodoma kwa asilimia 11 kutoka uzalishaji wa sasa.

“Jiji la Dodoma linazalisha nusu ya mahitaji ya maji ambapo mahitaji ni lita milioni 133 kwa siku na yanayozalishwa ni lita milioni 67 hivyo kuwa na upungufu wa lita milioni 66.7. Mradi huu unaenda kuongeza hali ya upatikanaji wa maji kwa siku.

“Huu ni uwekezaji mkubwa na sisi kamati ya bunge tunampongeza Rais Dk.Samia kwa kuwajali wananchi wa Tanzania hasa wanaoishi Dodoma kwasababu ni makao makuu ya nchi na shughuli nyingi za serikali zipo hapa na mahitaji ya maji yanaongezeka siku hadi siku,”

Aidha Sangu ameipongeza Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) kwa kutekeleza mradi huo ambao ukikamilika utapunguza kero ya maji kwa wananchi.

"Mradi huu unaendeshwa kwa njia ya kisasa kuanzia kwenye kusukuma maji, kutibu na kupima ujazo wa maji.Mfumo huu umetupa imani kama kamati kwasababu tulikuwa tunatamani sana kuona taasisi hizi zinakuwa na mifumo ya kisasa ambayo itasaidia kuzuia upotevu wa maji,”amesema Sangu



Nae Mkurugenzi wa (DUWASA) Mhandisi Aron Joseph amesema mradi huo umefikia asilimia 96 na ukikamilika utawanufaisha wananchi zaidi ya 75000.

Amesema mradi huo unatekelezwa kwa fedha za mapato ya ndani ambapo hadi sasa serikali imeshatoa sh bilioni 3 sawa na asilimia 71.

“Mradi huu utahudumia wananchu wa nzuguni na maeneo ya jirani. Baada ya awamu ya kwanza ya utekelezaji tumeanza kuchumba visima 11 na zoezi hilo limeanza rasmi lengo ni kuhakikisha tunaunga jitihada za Rais Dl.Samia za kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya maji,”amesema

Katibu Mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dodoma Jawadu Mohmed nae amesema CCM itakikisha kila nyumba ya mwananchi wa Dodoma inafikiwa na huduma ya maji.

Amesema dalili njema ni pamoja na kuona DUWASA wakiendelea na mikakati ya kuongeza uzalishaji wa maji ili watu wote wanufaike na huduma hiyo kwasababu haina mbadala.

“Tunaona jitihada zinazofanywa na DIWASA chini ya usimamizi wa serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dk.Samia shida ya maji inaenda kusiha kwasababu tunaona mikakati mizuri ambayo imewekwa,”amesema

No comments:

Post a Comment