 |
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (Kulia), akiitambulisha rasmi Tovuti ya Taasisi ya Usuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi (Tax Ombudsman Service Tanzania – TOST-www.tos.go.tz), wakati wa Uzinduzi rasmi wa Taasisi hiyo katika ukumbi wa Kambarage, Wizara ya Fedha, Dodoma. Hafla hiyo imehudhuriwa na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, Viongozi wa Taasisi mbalimbali za Serikali, Viongozi wa Wizara ya Fedha, Viongozi wa Dini, Taasisi zisizo za Kiserikali pamoja na wanahabari. |
 |
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (Kushoto), akimkabidhi mwongozo wa Sheria ya Usimamizi wa Kodi, Sura ya 438 kwa Msuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi, Bw. Robert Manyama, baada ya kuzindua Taasisi ya Usuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi (Tax Ombudsman Service Tanzania – TOST), katika ukumbi wa Kambarage, Wizara ya Fedha, Dodoma. Taasisi ya Usuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi ni chombo huru chenye jukumu la kupitia na kushughulikia malalamiko yote ya walipakodi kuhusu huduma, masuala ya kiutaratibu na kiutawala yanayoweza kujitokeza katika usimamizi wa sheria za kodi zinazotekelezwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA. |
 |
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akizungumza wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Taasisi ya Usuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi-TOST, iliyofanyika katika ukumbi wa Kambarage, Wizara ya Fedha, Dodoma. Taasisi hiyo imeanzishwa baada ya Bunge la Tanzania, tarehe 13 Juni 2019, kupitisha Sheria ya Fedha ya mwaka 2019, iliyoanza kutumika tarehe 1 Julai 2019, ambapo Sheria hiyo ilifanyiwa marekebisho Sheria ya Usimamizi wa Kodi, Sura ya. 438 ili kuanzisha Taasisi hiyo inayojulikana kama “Taasisi ya Usuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi – Tax Ombudsman Service Tanzania”. |
 |
Msuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi, Bw. Robert Manyama, akizungumza wakati akimkaribisha Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (hayupo pichani), wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Taasisi ya Usuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi-TOST, iliyofanyika katika ukumbi wa Kambarage, Wizara ya Fedha, Dodoma. Taasisi hiyo imeanzishwa baada ya Bunge la Tanzania, tarehe 13 Juni 2019, kupitisha Sheria ya Fedha ya mwaka 2019, iliyoanza kutumika tarehe 1 Julai 2019, ambapo Sheria hiyo ilifanyiwa marekebisho Sheria ya Usimamizi wa Kodi, Sura ya. 438 ili kuanzisha taasisi hiyo inayojulikana kama “Taasisi ya Usuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi – Tax Ombudsman Service Tanzania”. |
 |
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (hayupo pichani), wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Taasisi ya Usuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi-TOST, iliyofanyika katika ukumbi wa Kambarage, Wizara ya Fedha, Dodoma. Taasisi hiyo imeanzishwa baada ya Bunge la Tanzania, tarehe 13 Juni 2019, kupitisha Sheria ya Fedha ya mwaka 2019, iliyoanza kutumika tarehe 1 Julai 2019, ambapo Sheria hiyo ilifanyiwa marekebisho Sheria ya Usimamizi wa Kodi, Sura ya. 438 ili kuanzisha Taasisi hiyo inayojulikana kama “Taasisi ya Usuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi – Tax Ombudsman Service Tanzania”. |
 |
Viongozi mbalimbali wa Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Fedha, wakifuatilia kwa umakini halfa ya Uzinduzi wa Taasisi ya Usuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi-TOST, iliyofanyika katika ukumbi wa Kambarage, Wizara ya Fedha, Dodoma. Taasisi hiyo imeanzishwa baada ya Bunge la Tanzania, tarehe 13 Juni 2019, kupitisha Sheria ya Fedha ya mwaka 2019, iliyoanza kutumika tarehe 1 Julai 2019, ambapo Sheria hiyo ilifanyiwa marekebisho Sheria ya Usimamizi wa Kodi, Sura ya. 438 ili kuanzisha taasisi hiyo inayojulikana kama “Taasisi ya Usuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi – Tax Ombudsman Service Tanzania”. |
 |
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akibofya kuonesha Nembo rasmi ya taasisi hiyo kama ishara ya kuzindua Taasisi ya Usuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi-TOST, iliyofanyika katika ukumbi wa Kambarage, Wizara ya Fedha, Dodoma. Taasisi hiyo imeanzishwa baada ya Bunge la Tanzania, tarehe 13 Juni 2019, kupitisha Sheria ya Fedha ya mwaka 2019, iliyoanza kutumika tarehe 1 Julai 2019, ambapo Sheria hiyo ilifanyiwa marekebisho Sheria ya Usimamizi wa Kodi, Sura ya. 438 ili kuanzisha taasisi hiyo inayojulikana kama “Taasisi ya Usuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi – Tax Ombudsman Service Tanzania”. |
 |
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb)(katikati walioketi), Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, Bw. Daniel Sillo (wa pili kulia walioketi), Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Bi. Rosemary Senyamule (wa kwanza kushoto walioketi), Katibu wa Uchumi na Fedha wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Frank Haule (wa pili kushoto walioketi) na Msuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi, Bw. Robert Manyama (wa kwanza kulia walioketi), wakiwa katika picha ya pamoja na Watumishi wa Taasisi ya Usuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi-TOST, baada ya kumalizika kwa hafla ya Uzinduzi wa Taasisi hiyo, uzinduzi uliofanyika katika ukumbi wa Kambarage, Wizara ya Fedha, Dodoma. |
 |
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (katikati walioketi), Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, Bw. Daniel Sillo (wa pili kulia walioketi), Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Bi. Rosemary Senyamule (wa kwanza kushoto walioketi), Katibu wa Uchumi na Fedha wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Frank Haule (wa pili kushoto walioketi) na Msuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi, Bw. Robert Manyama (wa kwanza kulia walioketi), wakiwa katika picha ya pamoja na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, baada ya kumalizia kwa hafla ya Uzinduzi wa Taasisi hiyo, iliyofanyika katika ukumbi wa Kambarage, Wizara ya Fedha, Dodoma. |
 |
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (katikati walioketi), Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, Bw. Daniel Sillo (wa pili kulia walioketi), Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Bi. Rosemary Senyamule (wa kwanza kushoto walioketi), Katibu wa Uchumi na Fedha wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Frank Haule (wa pili kushoto walioketi) na Msuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi, Bw. Robert Manyama (wa kwanza kulia walioketi), wakiwa katika picha ya pamoja na Menejimenti ya Wizara ya Fedha, baada ya kumalizia kwa hafla ya Uzinduzi wa Taasisi hiyo, iliyofanyika katika ukumbi wa Kambarage, Wizara ya Fedha, Dodoma. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Dodoma |
Na Debora Lemubi, Dodoma.
Wito umetolewa kwa Wauzaji wa bidhaa Nchini kuwa na Utamaduni wa kutoa Risiti na kwa Wanunuzi pia kuwa Utaratibu huo wa kudai Risiti pindi wafanyapo manunuzi kwani kinyume chake ni kuahirisha tatizo, kwani kwa kufanya hivyo kutakuwepo mizozo katika suala la ulipaji wa Kodi.
Wito huo kwa Wanunuzi na Wauzaji wa bidhaa umetolewa na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Mwigulu Lameck Nchemba mapema leo hii Jijini Dodoma, katika Uzinduzi wa Taasisi ya Usuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi ambayo imekuwa ni moja ya maono ya muda mrefu ya Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Dkt Samia Suluhu Hassan.
"Huku watu wanaouza bidhaa watoe risiti,na watu wanaonunua bidhaa wadai risiti yeyote ambaye ataacha kufanya hivyo anaahirisha tatizo tu lakini huko mbele atakutana na mkono wa Sheria,tusiahirishe tatizo tufuate Sheria ili tusiingie kwenye mizozo isiyostahili".
Sambamba na hayo Waziri Nchemba ameitaka Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) kutofanya mzaha na wale wanaokiuka sheria,na kuhakikisha mtu analipa Kodi stahiki.
"Kwahiyo TRA Wala msifanye mchezo na mtu anayekiuka Sheria,mtun anayekiuka Sheria msifanye mchezo nae, Zingatieni Sheria,Zingatieni Weledi, Zingatieni mtu alipe Kodi stahiki msimbambikizie mtu Kodi alipe Kodi anayostahili".
Pia Waziri amesema kuwa Takwimu za walipa Kodi za Nchi yetu bado hazituweki pazuri na uwiani bado ni changamoto.
"Ukienda kwenye Takwimu za Nchi yetu za walipa Kodi,ukienda kwenye Takwimu zote hazituweki pazuri Sana,ukiangalia uwiano wa Kodi ukaweka kwenye lesho ya GDP ya pato letu uwiano bado uko chini".
Awali akitoa salami za Mkoa, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mh Rosemary Senyamule amesema kuwa kuanzishwa kwa Taasisi hii kutapunguza Malalamiko waliyokuwa wanayapata kutoka kwa wafanya biashara kwani wamepata pa kuyapeleka.
"Najua Taasisi hii itakuwa na mchango mkubwa wa kutupunguzia sisi kero ambazo tumekuwa tukizipokea kutoka kwa wafanya biashara,kwani wamepata mahali pa kuzipeleka".
Naye Msuluhishi Bwana Robert Manyama amesema mikakati ya kutoa elimu kwa Umma kupitia vyombo mbalimbali vya habari itazingatiwa.
"Hivyo mikakati ya utiaji Elimu kwa Umma kupitia vyombo mbalimbali vya habari ikiwemo mitandao ya kijamii utazingatiwa tukishirikiana na wadau wetu mbalimbali".
Kwa upande wake Mwenyekiti Kamati ya kudumu ya Bunge la Bajeti Mh Daniel Silo umuhimu wa uwepo wa uwazi katika utekelezaji wa majukumu ndani ya Taasisi hiyo Ila kupata mafanikio.
"Mimi niendelee kusisitiza suala la uwazi katika kutekeleza majukumu ndani ya Taasisi ili kupunguza Malalamiko yasiyo ya lazima".
Taasisi hii imekuwa ni hitajio kubwa la Nchi, kwa Watanzania na hata Serikali kwa ujumla chini ya Mh Dkt Samia Suluhu Hassan Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
No comments:
Post a Comment