Mhe. Aweso katika ziara hiyo ameambatana na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule, Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Mkoa na Wilaya ya Dodoma, Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maji, Mhandisi Mwajuma Waziri, Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira (DUWASA), wataalamu kutoka Wizara ya Maji, Mkurugenzi Mtendaji wa DUWASA Mhandisi Aron Joseph na Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Mhandisi Clement Kivegalo
Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) amefanya kikao kifupi katika ofisi ya mkuu wa mkoa wa Dodoma kabla ya kuanza ziara katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kufuatilia hali ya upatikanaji wa huduma ya majisafi katika chuo hicho chenye wanachuo wapatao elfu 33.
No comments:
Post a Comment