BUNGE LAPITISHA MISWADA MITATU YA UCHAGUZI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, February 2, 2024

BUNGE LAPITISHA MISWADA MITATU YA UCHAGUZI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama akitoa ufafanuzi kuhusu hoja za wabunge zilizowasilishwa wakati wa majadiliano ya miswada ya sheria ya uchaguzi katika Bunge linaloendelea Jijini Dodoma tarehe 02, 2024.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi akitambulishwa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson wakati alipohudhuria Bunge la 12 Mkutano wa 14 kikao cha Nne tarehe 02, Februari 2024 Jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi (kulia) akiteta jambo na Naibu wake Bw. Anderson Mutatembwa wakati wa Bunge linaloendelea Jijini Dodoma tarehe 02 Februari, 2024.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Ummy Nderianana akichangia maoni yake kuhusu miswada ya sheria ya uchaguzi wakati wa Bunge linaloendelea Jijini Dodoma tarehe 02 Februari, 2024
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama (wa tatu kulia) na Naibu Wake Mhe. Ummy Nderiananga wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watendaji wa fisi yake mara baada ya kupitishwa kwa miswada ya sheria ya Uchaguzi katika Bunge linaloendelea Jijini Dodoma tarehe 02, Februari 2024.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Ummy Nderianana akizungumza na Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Dkt. Jim Yonazi mara baada ya kupitishwa kwa miswada ya sheria ya Uchaguzi katika Bunge linaloendelea Jijini Dodoma tarehe 02, Februari 2024.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama akiteta jambo na Katibu Mkuu wa Ofisi yake Dkt. Jim Yonazi mara baada ya kupitishwa kwa miswada ya sheria ya Uchaguzi katika Bunge linaloendelea Jijini Dodoma tarehe 02, Februari 2024.

(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

Na Mwandishi Wetu , Dodoma 

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limepitisha muswada wa sheria ya Tume ya Taifa ya uchaguzi, muswada wa sheria ya uchaguzi wa Rais, wabunge na madiwani na muswada wa sheria ya marekebisho ya sheria ya vyama vya siasa.

Miswada hiyo mitatu imepitishwa mara baada ya kujadiliwa na wabunge katika mkutano wa 14 wa Bunge linaloendelea Jijini Dodoma Februari 02, 2024 ambapo Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Jenista Mhagama alitoa ufafanuzi kuhusu hoja za wabunge zilizowasilishwa wakati wa majadiliano ya miswada ya sheria ya uchaguzi.

No comments:

Post a Comment