DRC YATAKA KUREJESHA ADHABU YA KIFO KWA WANAJESHI WANAOPATIKANA NA HATIA YA UHAINI. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, February 12, 2024

DRC YATAKA KUREJESHA ADHABU YA KIFO KWA WANAJESHI WANAOPATIKANA NA HATIA YA UHAINI.



Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ina lengo la kurejesha adhabu ya kifo, ambayo ilisitishwa miaka 20 iliyopita, kwa wanajeshi wanaopatikana na hatia ya uhaini dhidi ya waasi wa M23, kulingana na ripoti ya baraza la mawaziri.

Hukumu za kifo hutolewa mara kwa mara na mahakama nchini DRC lakini zilibadilishwa kuwa za kifungo cha maisha gerezani tangu kuondolewa kwa hukumu ya kifo mwaka wa 2003.

Waziri wa sheria aliwasilisha barua kwa baraza la mawaziri kuhusu “kuondoa katazo la hukumu ya kifo kwa wanajeshi”, msemaji wa serikali Patrick Muyaya alisema.

Alisema “Katika lengo la kukomesha uhaini, Baraza la ulinzi lilimuomba Rais kuondoa katazo hilo kipindi hiki ambapo, nchi inakabiliwa na uchokozi kutoka Rwanda,” ambayo inakanusha madai ya kuwasaidia waasi wa M23.

Baada ya miaka mingi ya utulivu, M23 (Movement ya Machi 23) ilichukua tena silaha mwishoni mwa 2021 na tangu wakati huo imeteka maeneo makubwa ya jimbo la Nord Kivu.

Baada ya utulivu wa uchaguzi wa Desemba 20, ambao ulimrejesha Rais Felix Tshisekedi kwa muhula wa pili, mapigano yameanza tena na kusababisha vifo vya watu kadhaa na maelfu ya wengine kuyahama makazi yao.

"Kwa kuzingatia hitaji kamili ... kuondoa jeshi la wasaliti kwa kutekeleza adhabu ya kifo wanayostahili baada ya hukumu isiyoweza kutenduliwa kwa uhaini," wizara ya sheria iliomba serikali "kutambua nia ya kuondoa kusitishwa," msemaji huyo alisema.

No comments:

Post a Comment