![]() |
Msajili wa Bodi ya Makandarasi (CRB)Mhandisi Rhoben Nkori ,akizungumza na waandishi wa habari leo Februari 8,2024 Jijini Dodoma na kutoa taarifa ya uchunguzi wa ajali ya kuvunjika kwa Kalavati katika barabara ya Kanyinabushwa Mbale “A” iliyoko Wilaya ya Misenyi mkoani Kagera. |
Na Okuly Julius ,DODOMA
Kufuatia
maeelekezo yaliyotolewa na Waziri wa
Ujenzi Innoncent Bashungwa mnamo Januari 17,2024 baada ya ajali ya kuvunjika
kwa Kalavati katika barabara ya Kanyinabushwa Mbale “A” iliyoko Wilaya ya
Misenyi mkoani Kagera, Bodi ya Usajili wa Makandarasi (CRB) Pamoja na Bodi ya
Usajili wa Wahandisi (ERB) zimetoa taarifa za uchunguzi wa ajali hiyo na
kumtaka mkandarasi kurudia ujenzi wa Kalvati hilo kwa gharama zake.
Taarifa hiyo
imetolewa leo Februari 8,2024 Jijini Dodoma na Msajili wa Bodi ya Wahandisi Mhandisi
Benard Kavishe mbele ya wanahabari na kuongeza kuwa mapungufu yaliyosababisha
uharibifu huo yalisababishwa na mkandarasi hivyo wamemchukulia hatua stahiki
kwa mujibu wa sharia ya Usajili wa Wakandarasi sura ya 35 ya mwaka 2002.
“ERB na CRB
ziliunda timu ya Wataalamu kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa ajali hiyo ambapo
timu ilichukua hatua ya kutembelea mradi huo Jnauari 20,2024, kufanya mahojiano
na TARURA mkoa wa Kagera,Msimamizi wa mradi na mkandarasi,kupitia nyaraka za
mradi huo na kuandaa ripoti ya uchunguzi iliyobainisha chanzo cha kubomoka kwa
daraja dogo na kupendekeza hatua stahiki” amesema Mhandisi Kavishe
Ambapo
Mhandisi Kavishe amebainisha matokeo ya uchunguzi huo kuwa ni kutozingatiwa kwa
matakwa ya mkataba ,hasa uwepo wa wataalamu walioainishwa, kutumika kwa
malighafi hafifu kinyume na matakwa ya mkataba na kuruhusu kupita kwa vyombo
vya moto kabala ya Kalvati kukamilika ujenzi wake.
Kwa upande
wake Msajili wa Bodi ya Makandarasi Mhandisi Rhoben Nkori amewataka wadau wa
sekta ya ujenzi kwa ujumla kuzingatia Sheria ,Kanuni na Miongozo katika
utekelezaji wa miradi.
Ikumbukwe
kuwa Mkandarasi EACI Company Ltd ndio alikuwa anatekeleza ujenzi wa mradi huo
ambapo tayari ameshachukuliwa hatua za kisheria na Bodi zote mbili ikiwemo kutakiwa kurudia ujenzi wa
mradi huo kwa gharama zake mwenyewe ili wananchi waanze kutumia Kalvati hiyo kw
utekelezaji wa shughuli zao za kila siku.
No comments:
Post a Comment