Na Carlos Cloudio, OKULY BLOG, DODOMA
Kampuni ya Bidhaa Taka ya Hadija (Hadija Waste Products Management) imeweza kupiga vita uchafuzi wa mazingira kwa kurejeleza taka zijulikanazo kama mali taka zinazopatikana jijini Dodoma ambazo hutokana na matumizi ya awali kupitia bidhaa hizo.
Menejimenti hiyo ya Hadija pia imekuwa mchango mkubwa kwa vijana katika sekta ya ajira na zaidi ya vijana 10 kutoka matawi tofauti wamekuwa wakipata kipato kupitia menejimenti hiyo ya Hadija inayojihusisha na ukusanyaji taka kabla ya uchakataji.
Akizungumza leo Ijumaa, Februari 2, 2024 na OKULY BLOG jijini Dodoma, meneja wa vifaa Abdul Karim amesema kampuni ya Bidhaa Taka ya Hadija imekuwa mfano jijini Dodoma kwa kusafisha mji pamoja na kugawa ajira kwa vijana kwani kampuni imerasimishwa na inafanya biashara kihalali wakiwa wamepokea vibali na leseni na wanalipa kodi kama ilivyo kampuni zingine.
“Unapoongelea Hadija Waste Products Management ni sehemu ambayo imerasimishwa na ipo kihalali na tuna vibali pamoja na leseni ambayo tunalipia jiji tukiwa tumeshapata kibali cha kulipia TRA pia tuna unga mkono serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na tunatoa ajira kwasababu kila siku vijana zaidi ya 10 wanafanya kazi hapa lakini sio hapa tu kwani tuna matawi tofauti jijini Dodoma yanayopatikana Chamwino, Makulu, Chaduru na Kikuyu,”amesema Karim.
Amesema pamoja na changamoto ya biashara hiyo anapenda kushauri kundi la vijana kujishughulisha na kutokaa mitaani pamoja na vijiweni kwa kusingizia ajira ni ngumu huku wakipoteza muda na kujiingiza katika makundi mabaya.
Amesema lengo la kuanzishwa kwa kampuni hiyo ni kusaidia kundi la vijana ambao wapo mtaani kwa ukosefu wa ajira pamoja na kuweka jiji safi na tangu waanze kukusanya bidhaa taka mitaani imepelekea jiji kuwa safi na kukosekana makopo yanayozagaa mitaani.
“Maisha ni magumu sana na kama kijana lazima upambane uwe na juhudi nyingi ndio maana tunahamasisha vijana kama hauna ajira, hauna elimu hauna haja ya kukaa mtaani na vijiweni cha kufanya tafuta hizi bidhaa ambazo tunazihitaji na utuletee hapa Hadija Waste Products tunaopatikana Majengo na utapata pesa yako kwa uharaka na maisha yanaendelea kwani vijana wengi sana hapa wanapambana na kwa siku wapo wanaoingiza shilingi elfu 50 na wengine elfu 40 hadi 30 pamoja na kwa kufanya hivyo tunakuwa tumeisaidia serikali yetu kwa kuweka jiji safi.
Kwa upande wa kijana Abdala Jumanne Alli amesema biashara imekuwa na manufaa kwa upande wake kwani imechangia kuongeza kipato licha ya changamoto ambazo anapitia wakati wa ukusanyaji wa makopo mtaani jamii imekuwa ikimchukulia tofauti na kumdharau lakini binafsi anatambua faida ya kazi hiyo kwa kipato na utunzaji wa mazingira kutokana na kundi la vijana kuokota bidhaa taka hizo imepelekea kutokuwa na uzagaaji wa rasilimali taka hizohasa makopo mitaani.
No comments:
Post a Comment