Na Okuly Julius ,Dodoma
WAZIRI
wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa ujasiri na uwezo mkubwa katika kusimamia
miundombinu ikiwemo ujenzi wa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Msalato Dodoma.
Prof. Mbarawa ametoa kauli hiyo
Februari 7,2024 jijini Dodoma , wakati alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya
ujenzi wa Mradi wa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Msalato.
“Tunamshukuru sana Rais Samia
Suluhu Hassan amekuwa ni mjasiri na uwezo mkubwa katika kusimamia miundombinu,
Wizara ya Uchukuzi tunamshukuru sana, leo tumesimama katika lami ya kiwanja cha
ndege cha Msalato,” amesema Mbarawa
Pia Prof. Mbarawa amewataka wakandarasi kujipanga ili mradi huo ukamilike
kwa wakati na watanzania waone kwa vitendo kazi inayofanywa na serikali.
“Hakuna shida ya fedha, fedha zipo
mkandarasi atoe certificate ili tuweze kumlipa lakini kuna changamoto za mvua
ni vyema mkatengeneza mpango kazi kuhakikisha mradi unakamilika kama
ulivyopangwa Mei mwakani,” amesisitiza Mbarawa
Amesema kuwa ujenzi huo umekamilika
kwa asilimia 47 upande wa miundombinu na
asilimia 12.4 upande wa majengo.
Amesema kuwa mradi huo unajengwa
kwa thamani ya Sh bilioni 354, kati ya hizo Sh bilioni
164 kwa ajili ya njia ya kutokea ndege ,maegesho , kuingilia ndege
na Sh bilioni 194 kwa ajili ya jengo la abiria.
Amesema
kuwa uwanja huo ni mkubwa utakuwa na kilomita 3.6.
“Utakuwa na sifa za pekee ya kuwa
na vifaa vya kisasa vya kuongozea ndege, mfumo wa kuruhusu ndege kutua masaa 24
kuwe na mvua ,jua au ukungu ndege itatua tofauti na viwanja vingine,
Pia
uwanja huo utaweza kuchukua ndege kubwa kama aina ya Air bus.
Amesema kwa upande wa majengo,
jengo litakuwa na uwezo wa kuchukua abiria milioni 1.5 kwa mwaka, na kutakuwa
na mfumo wa kuongozea ndege wenye urefu wa mita 56 sawa na ghorofa 16.3,
utakuwa ni uwanja mzuri na wa kisasa.
Kwa upande wake, Meneja wa Wakala
wa Barabara Tanzania (TANROADS) mkoa wa Dodoma, Zuhura Amani amesema kuwa katika
utekelezaji wa mradi wa miundombinu mradi utakuwa na maegesho ya
magari 500, uzio ukubwa wa kilomita 37 mradi ulisainiwa Septemba 2022,kwa
gharama ya Sh bilioni 165.6 mkataba wa miezi 36 mradi
ulianza Aprili 2022 na utakamilika Aprli 2025.
Pia amesema utekelezaji
wa mradi wa miundombinu umefikia asilimia 47.9, mradi umeajiri wafanyakazi 495
kati ya hao 464 ni Watanzania.
Amesema mradi wa majengo utahusisha
ujenzi wa jengo la abiria lenye uwezo wa kuhudumia abiria milioni 1.5 kwa
mwaka,ujenzi wa jengo la kuongoza ndege, usimikaji wa vifaa vya mfumo wa
kuongozea ndege, ujenzi wa jengo la zimamoto, lenye uwezo wa kuhudumia ndege
daraja la 4E na mifumo wa kuongozea ndege, kituo cha kufua umemne,
jengo la hali ya hewa na usimikaji wa mitambo yake.
Amesema mkandarasi amesaini mkataba
kwa gharama ya Sh bilioni 194.4 bila ongezeko la kodi , mkataba ulianza Novemba
2022, utakamilika Novemba 2025, utekelezaji wa mradi umefikia asilimia 12.4,
ambapo kuna jumla ya wafanyakazi 389 kati ya hao 359 ni Watanzania.
Amesema kuwa mradi huo unafadhiliwa
na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Benki ya Maendeleo ya Afrika
(AfDB)
Amesema
kuwa jumla ya wananchi 1,772 walilipwa kiasi cha Sh bilioni 14.9
kama fidia ya kupisha eneo hilo.
Amesema
kuwa kumekuwwepo na changamoto ya mvua katika utekelezaji wa mradi lakini
wameweka mikakati kuhakikisha mradi unakamilika kama ilivyopangwa.
Kwa upande wake Katibu Mwenezi wa
Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Dodoma Jawadu Mohamed alisema kuwa ilani ya
CCCM imekuwa ikitekelezwa kwa vitendo katika mkoa wa Dodoma.
Amesema
kuwa wakati Rais Samia aliiingia madarakani wengi walikuwa na mashaka juu ya
ukamilishwaji wa miradi ikiwemo Mji wa Serikali, barabara za mzunguko na uwanja
wa ndege wa kimataifa wa Msalato Dodoma.
“Rais Samia amepambana kuhakikisha
akakamilisha kazi hizo, tumuunge mkono kiongozi huyu wan chi kwenye jitihada
kubwa anazofanya,” amesema
Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Dkt. Hamisi Mkanachi, ambaye alimwakilisha mkuu wa mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule aliwataka wakandarasi hao kuongeza nguvu, ikiwemo nguvu kazi ili mradi huo ukamilike kwa wakati.
No comments:
Post a Comment