YANGA SC, KARIMJEE MOBILITY WAINGIA MAKUBALIANO. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, February 22, 2024

YANGA SC, KARIMJEE MOBILITY WAINGIA MAKUBALIANO.



Na Carlos Claudio,

Klabu ya Yanga SC imeingia makubaliano na kampuni ya Karimjee Mobility kupitia kampuni ya Hero inayojihusisha na utengenezaji pamoja na usambazaji wa pikipiki.

Kampuni hiyo kutoka India inayofanya biashara na zaidi ya mataifa 40 imesaini mkataba wa Tsh milioni 300 ambao utadumu kwa kipindi cha miezi 18.

Akizungumza leo Februari 22, 2024 na waandishi wa habari jijini Dar-Es-Salaam katika makao makuu ya klabu Jangwani, raisi wa klabu ya Yanga SC Injinia Hersi Said amesema yafwatayo.

"Leo tumeingia makubaliano na kampuni ya Karimjee Mobility kupitia kampuni ya Hero ambayo inatengeneza pikipiki na kusambaza. Kampuni ya Hero inatajwa kuwa kampuni namba 1 duniani kwa biashara hiyo. Kampuni hii kutoka India inafanya biashara mataifa zaidi ya 40. Young Africans SC itapata kiasi cha Tsh Milioni 300 kutoka kwenye mkataba huu katika kipindi cha miezi 18.

"Mkataba huu utaruhusu kwa matawi yetu ya Klabu kupata posho kwenye mauzo ya pikipiki hizo. Kwahiyo kila tawi linapaswa kuhakikisha biashara hi inakuwa kwa kasi. Hivyo basi kila mwananchi pikipiki yako ya kununua ni Hero na pikipiki ya kutumia ni Hero.

"Tuwahakikishie kampuni ya Hero kuwa Sisi ni Klabu namba moja na tutahakikisha Hero ambao ni namba moja waendelee kubakia kuwa namba moja. Uwezo wa kuifanya Hero kuwa namba moja ni jukumu la kila Mwanachama wa Young Africans, hivyo kuanzia sasa bodaboda ni Hero,"Hersi Said.

Ushirikiano huu wa kibiashara kwa kipindi cha miezi 18, unakuwa ni wa mfano na wa kuvutia ambao Yanga SC na matawi yake kote nchini Tanzania watafanya kazi kama mtandao wa usambazaji wa pikipiki a HERO

Kwa upande wa Meneja Masoko wa Karimjee Mobility Nadah Dhiyeb alisema: "Tunajivunia kuingia mkataba na klabu yenye heshima kubwa sana katika historia ya soka la Tanzania. Tunajua muungano huu kupitia Matawi ya Yanga SC tutapanua wigo wa biashara yetu kwa kuweka mtandao mkubwa."

"Watu 10 wa kwanza kununua Hero watapata huduma ya pikipiki (services) mara tatu bure. Vile vile wanatoa bima ya dereva na mtaji wake. Utajipatia vile vile helmet yenye nembo ya Young Africans SC"Ally Kamwe.

No comments:

Post a Comment