ACHANENI NA UHALIFU ENDELEZENI MATENDO YA HURUMA. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Sunday, March 31, 2024

ACHANENI NA UHALIFU ENDELEZENI MATENDO YA HURUMA.


"Afichaye dhambi zake hatafanikiwa, Bali yeye aziungamaye na kuziacha atapata rehema"Mithali 28:13-14.

Nukuu hii ya maneno haya kutoka katika Biblia takatifu yamesemwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Theopista Mallya wakati akitoa salamu za sikukuu ya Pasaka katika Kanisa la kiinjili la kilutheri Tanzania Dayosisi ya Dodoma Jimbo la Makao Makuu ushirika wa Arusha road.

Kamanda Mallya amesema kupitia sikukuu hii waumini wa dini kikristo walikuwa katika kipindi cha mfungo,  kufanya toba na matendo ya huruma, endeleeni kumcha mungu na kuacha dhambi".

Aidha, Kamanda Mallya amewataka waumini wa dini hiyo kuepuka kujichukulia sheria mkononi na kufanya vitendo vya kikatili kwa binadamu mwenzie hususani matukio ya mauaji na kukatisha uhai wa mtu jambo ambalo ni kinyume na sheria.

"Mwenye mamlaka ya kukatisha uhai wa mtu ni Mungu peke yake, hivyo kupitia maungamo na sala mlizofanya katika kipindi cha mfungo Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma hatutegemei kuwepo kwa matukio ya mauaji pamoja na uhalifu mwingine."amesema Kamanda Mallya.

Jeshi la polisi mkoa wa Dodoma limeshiriki ibada ya pamoja March 31, 2024 na waumini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Dayosisi ya Dodoma pamoja na kushiriki harambee.


Toka Dawati la Habari Dodoma.

No comments:

Post a Comment