BASHUNGWA ASHIRIKI MISA YA PASAKA JIMBONI KARAGWE. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Sunday, March 31, 2024

BASHUNGWA ASHIRIKI MISA YA PASAKA JIMBONI KARAGWE.


Waziri wa Ujenzi na Mbunge wa Jimbo la Karagwe, Innocent L. Bashungwa ameungana na Waumini wa Parokia teule ya Kayungu Jimbo Katoliki la Kayanga wilayani Karagwe kushiriki Misa Takatifu ya Pasaka, leo tarehe 31 Machi 2024.

Misa hiyo Takatifu imeongozwa na Padre Abdon Burondo, Mlezi wa Kituo cha Malezi Chabalisa ambapo wameshiriki waumini mbalimbali ikiwa ni pamoja na familia ya Waziri Bashungwa.

Waziri Bashungwa ametumia nafasi hiyo kutoa salamu za Serikali ya Awamu ya sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

No comments:

Post a Comment