ANGELLA OKUTOYI ANYAKUA MEDALI YA DHAHABU. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, March 22, 2024

ANGELLA OKUTOYI ANYAKUA MEDALI YA DHAHABU.




Mchezaji tenisi wa Kenya Angella Okutoyi aliendeleza matumaini yake kuelekea kufuzu kwa Mashindano ya Tenisi ya Olimpiki ya Paris 2024 baada ya kushinda dhahabu kwa wanawake katika Michezo ya Afrika mjini Accra, Ghana.


Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 alimshinda Lamis Elhussein Abdelaziz, wa Misri, 6-4 6-2. Nafasi hiyo, hata hivyo, itaimarishwa tu ikiwa Okutoyi ataorodheshwa na Shirikisho la Tenisi Duniani, WTA kuwa miongoni mwa wachezaji bora 400 duniani kufikia Juni 10, tarehe ya mwisho ya mchujo wa Mashindano ya Tenisi ya Olimpiki.


Okutoyi ambaye kwa sasa anaorodheshwa nambari 532 duniani bado ana kazi ya kufanya ili kujihakikishia nafasi mjini Paris, ambapo anaweza kuwa mwanamke wa kwanza Mkenya katika historia kucheza katika Mashindano ya Tenisi ya Olimpiki.


"Kufuzu kwa Olimpiki kunamaanisha mengi kwangu. Imekuwa ndoto yangu tangu nikiwa mdogo,” alisema Okutoyi.


"Tangu niliposhika racket nimekuwa nikitazama Olimpiki kwenye TV, kwa hivyo nina furaha kubwa kuweza kutimiza hilo leo.” “Hii itakuwa na maana kubwa kwa tenisi nchini Kenya na kwa bara la Afrika. Nina furaha kwamba niliweza kushinda leo na ninataka tu kuendelea na kuendelea.”

No comments:

Post a Comment