Na Okuly Julius-Dodoma
Ametoa maagizo hayo Leo Machi 22, 2024 Jijini Dodoma , wakati wa maadhimisho ya kilele cha wiki ya maji na siku ya maji duniani.
Amesema kuwa katika kuhakikisha kunakuwa na uhakika wa upatkanaji maji mamlaka za maji zinatakiwa kusimamia vizuri miradi ya maji ili kuwe na uhakika wa upatikanaji wa maji.
Ametaja maagizo hayo kuwa ni pamoja na Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 kuendelea kutoa maoni kuhusu uhifadhi wa maji
Pia kulinda vyanzo vya maji,Taasisi za bonde na Baraza la Taifa la Uhifadhi wa Mazingira (NEMC) kuongeza jitihada za kudhibiti uchafuzi wa mazingira ili yasiathirike kushirikiana kwenye suala la kuangalia uwekezaji kwenye miradi inayotaka kufanyika.
“Sekta binafsi kuendelea kushirikiana na serikali katika kuhakikisha upatikanaji wa majisafi na salama. Pia viongozi na wataalam kushirikiana katika kulinda vyanzo vya maji,” amesema
Maagizo mengine ni kila kaya, taasisi kuweka miundombinu ya kuvuna maji, Taasisi za serikali zishirikiane katika kuhakikisha uhifadhi wa mazingira na maji unakua endelevu
“Baadhi ya vyanzo vya maji vilivyovamiwa virudishwe, kuendelea kutoa maoni kwenye mkakati wa kuhifadhi vyanzo vya maji, kuona tatizo kwa ukubwa kama taifa,” amesema
Maagizo mengine Watazania wapate huduma ya maji safi na salama kulinda vyanzo vya maji, kwenye maeneo yasiyo na vyanzo kuwe na miradi ya kimkakati.
Pia Wizara ya maji ijengee uwezo wa wataalam wake wa kuandaa maandiko ili fedha za mazingira ambazo ni nyingi Tanzania inufaike.
Vile vile, sekta ya maji ihakikishe inatenga fedha ili kuhakikisha mipango ya hifadhi inatekelezwa
“Miradi 1633 imekamilika, Rais ametoa fedha simamieni vizuriili wananchi apate maji ya uhakika,” amesema.
Amesema kuwa Rais amekua kinara wa kumtua Mwanamke ndoo kichwani kwa vitendo kwa kutoa fedha na kufuatilia utekelezaji wa miradi
“Aweso amekuwa muarobaini wa miradi ya maji ambayo ilikuwa imeshindwa kukamilika kwa miaka mingi,” amesema
Amesema kuwa ili maji yapatikane kuna uhusiano mkubwa na uhifadhi wa mazingira, ni muhimu kujiuliza tumeweka jambo gani kulinda vyanzovya maji.
Kwa upande wake, Waziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema kuwa Wizara ya Maji na Wizara ya Nishati kama ni mkulima na mfugaji
“Wakurugenzi na watendaji wa Wizara ya Maji hakuna kisingizio, twendeni tukashughulikie kutatua kero kwa wananchi,
"Wizara ya Maji miaka ya nyuma ilikuwa wizara ya lawama, na Rais Samia Suluhu Hassan amesema hataki kusikia na kuona kinamama wanateseka juu ya maji, Rais hakutuacha aliendelea kutuunga mkono," amesema Aweso
Amesema kuwa kuna miradi ilijengwa tangu mwaka 1970 lakini ilikuwa ikishindwa kukamilika kutokana na ufinyu wa fedha.
“Leo bajeti ya Wizara ya Maji imeongezeka,maji yamefika hadi Jibondo Mafia watu wanakaa kisiwani kwenye miamba lakini Rais Samia alitoa maji mjini akapitisha baharini na sasa wananchi wanapata maji,”amesema
Amesema maeneo ya wafugaji kinamama walikuwa wakitembea kilomita 25 kutafuta maji lakini sasa maji yamepatikana.
“Kazi ambayo ilitakiwa kufanywa kwa miaka 10 lakini Rais ameifanya kwa miaka mitatu, kwa muda mfupi vijiji 9737 vimefikishiwa maji na kuna mitambo kila mkoa. Watendaji Wizara ya Maji tusitoboe mbeleko tufanye kazi ambayo Rais ametuheshimisha tutumie maadhimisho ya kilele cha wiki ya maji kujitathimini , tunapokuwa na maji toshelevu tunakuwa na uhakika wa uchumi na amani katika nchi.,” amesema
Amesema kuwa mabadiliko ya tabia za binadamu yanakausha vyanzo vya maji,ni lazima kulinda na kutunza vyanzo vya maji, si jambo la wizara ni kushirikisha jamii.
“Tunajenga bwawa la Farkwa na bwawa la Kidunda huo ndio uelekeo wetu,” alisema
Amesema kuwa Rais ametoa maelekezo miezi miwili mradi wa Same Mwanga maji yatoke sasa mradi uko asilimia 86 na mwezi Juni maji yatatoka.
“Tumepewa maelekezo na Rais Juni lazima maji yatoke, nguvu ya Wizara inahamia site kuhakikisha wananchi wa Same Mwanga wanapata maji safi na salama,” alisema
Naye, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Dk Selemani Jafo amesema kuwa kuna umuhimu mkubwa wa kutunza mazingira ikiwemo utunzaji wa mabonde ya maji.
Amesema kuwa kuna ajenda ya utunzaji mazingira kwa kupanda miti milioni 1.5 kila mkoa, ambapo kwa mwaka ni sawa na miti milioni 279, kwa mwaka huu tayari miti milioni 266 iliweza kupandwa katika Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini.
Katika kufanikisha utekelezaji wa miradi ya maji wizara ya maji imefanikiwa katika utoaji wa vyeti vya athari za kimazingira.
“Kuna kampeni mbalimbali ikiwemo soma na mti kwa wanafunziwa shule za msingi, sekondari na vyuo ili kuchagiza utunzaji wa mazingira,” amesema Dkt.Jafo
Awali ,Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega amesema kuwa hakuna shughuli za uhakika ukiwa hakuna maji.
“Tunaishukuru Wizara ya Maji kwa kuwezesha wafugaji kwa ujenzi wa mabirika ya kunyweshea mifugo ikiwemo miradi ya Longido , Wami Ruvu na kwingineko,” amesema
Amesema kuwa ni vyema kama Wizara kuendelea kusaidia katika kila mradi wa maji wanazingatia uwepo wa huduma ya mifugo.
Katibu Mkuu Wizara ya Maji,Mhandisi Rehema Waziri amesema kuwa malengo yaliyopo ni kuhakikisha upatikanaji wa maji unafikia asilimia 95 Mijini na asilimia 85 vijijini ifikapo mwaka 2025,ambapo kwa sasa upatikanaji wa maji kwa Mijini ni asilimia 90.1 na kwa vijijini ni asilimia 79.6
Mwakilishi wa Wadau wa Maendeleo Rehema Tukai amesema kuwa wataendelea kushirikiana na serikali katika kuhakikisha miradi ya maji na upatikanaji maji unakuwa na ufanisi.
Mwenyekiti wa Bodi ya Maji Taifa,Mhandisi Mbogo Mfutakamba amesema kuwa wamepiga hatua katika upatikanaji wa maji sasa wanajua mchango wa maji kwenye uchumi.
Naye Mjumbe wa NEC Donald Mejitii amesema kuwa katika mji wa Dodoma kazi ya usambazaji maji inaendelea vizuri kuhakikisha maji yanapatikana.
No comments:
Post a Comment