DKT. SAMIA AAHIDI KUBEBA AJENDA YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA BARANI AFRIKA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, March 9, 2024

DKT. SAMIA AAHIDI KUBEBA AJENDA YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA BARANI AFRIKA


Na Okuly Julius Dodoma

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Dkt Samia Suluhu Hassan amejitoa kuwa Kinara kwa kuibeba ajenda ya Matumizi ya Nishati safi ya kupikia Barani Africa.

Raisi Samia amesema hayo wakati alipozungumza kwa njia simu na wadau mbalimbali wakiwemo wanawake kutoka maeneo tofauti hapa Nchini katika Kongamano la wanawake la kugawa mitaji na vitendea kazi vya Nishati safi ya kupikia 2024 lililofanyika Leo Machi 9,2024 Jijini Dodoma.

Na kuongeza kuwa ahadi yake ni kuibeba Nchi kadri atakavyoweza katika suala hili.

"Mimi kiongozi wenu naibeba ajenda ya Nishati safi ya kupikia,ndani ya Bara la Africa Mimi ndio Champion wao".

"Lakini pia ahadi yangu kwa Wizara ya Mazingira kwako Makamu wa Raisi na Nishati pia,nitaibeba hiyo ajenda nikisaidiwa na ninyi,ni kwamba nitaibeba Nchi yetu kadiri nitakavyoweza kwenye suala hili".

Katika Hotuba yake Mgeni Rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Dkt Philip Mpango amesema kuwa hapa Tanzania Takribani hekta 469,420 za misitu hupotea kila mwaka kwa Shughuli za kibinadamu ikiwemo ukataji wa miti kwaajili ya kuni na mkaa hali inayopelekea uharibifu na hata kwenye vyanzo vya maji.

"Hapa Tanzania Takribani asilimia 90 ya kaya hutumia kuni na mkaa kama nyenzo kuu ya Nishati ambapo asilimia 65 ya Nishati inayotumika majumbani ni kuni, asilimia 26.2 ni mkaa na asilimia 8.8 ni mjumuisho wa gesi,umeme na vyanzo vingine".

"Kutokana na Matumizi Takribani hekta 469,420 za misitu hupotea kila mwaka kwa Shughuli za kibinadamu ikiwemo ukataji wa miti kwaajili ya kuni na mkaa,Hali hii huchangia kwa kiasi kikubwa uharibifu wa mazingira kupelekea hata kukauka kwa vyanzo vya maji".

Aidha Makamu wa Rais ameeleza kuwa wanawake ndio waathirika wakubwa wa matumizi ya Nishati chafu,kukutana changamoto katika utafutaji wa kuni ikiwemo vitendo vya ukatili wa kijinsia.

"Waheshimiwa viongozi na wadau wa Kongamano hili, wanawake ndio waathirika wakubwa wa matumizi ya Nishati chafu ya kupikia, inakadiliwa kuwa katika maeneo mengi ya vijijini wanawake wanatumia masaa 20 kwa wiki kutafuta kuni na hivyo kushindwa kujihusisha na Shughuli za Maendeleo lakini pia kuna changamoto nyingi wanazokutana nazo katika utafutaji wa kuni ikiwemo kukutana na nyoka na hata kukumbwa na vitendo vya ukatili wa kijinsia".

Naye Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt Ditto Biteko ametumia nafasi hiyo kuwaomba Wakuu wa Mikoa,Viongozi wa dini,Wababa katika familia zao na vyombo vya habari kutumia muda wanaoupata kuelezea umuhimu wa matumizi ya Nishati safi kwa watu wanaowazunguka.

"Hebu tuibebe hii ajenda kwa pamoja Wakuu wa Mikoa, Viongozi wa dini katika mahubiri yenu tafuteni sentensi mbili tatu kuwaambia waumini wenu umuhimu wa matumizi ya Nishati safi,wakina Baba nyumbani wakati mnazungumza na watoto wapeni sentensi mbili tatu wakue wakijua umuhimu wa matumizi ya Nishati safi".

Naye Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Ndg. Mary Chatanda (MCC) ameiomba Serikali kupunguza bei ya Nishati ya gesi ili wanawake Waweze kuachana na Matumizi ya kuni na mkaa kwenye shughuli za mapishi.

Amesema Bei ya Nishati safi ya Gesi ya kupikia ikipungua tofauti na ilivyo kwa sasa basi wananchi wengi wakiwemo wanawake wataweza kununua majiko na kuachana na Matumizi hatarishi ya kuni.

"Bei ya gesi ikipunguzwa madukani wanawake watakuwa na uwezo wa kununua kila yanapoisha na yatakuwa yanatumika nasio kuwa mapambo majumbani kwetu kama ilivyo sasa."

Na kuongeza " Ninaimani baada ya kongamano hili wanawake wote tuna kwenda kuwa mabalozi wazuri juu ya Matumizi ya nishati safi ya kupikia na sio kuni na mkaa," Amesema Chatanda.

Aidha amewapongeza waandaaji wa kongamano hilo ambao ni wizara ya Nishati kwa kuwaalika wanawake zaidi ya 10,000 kutoka mikoa tofauti tofauti na kuwapatia elimu na vitendea kazi vya nishati.

UWT imeahidi Kwenye ziara zake za Kata kwa Kata inakwenda kuhamasisha matumizi sahihi ya gesi safi ya kupikia kwa wanawake wote kuachana na kuni ili kutunza mazingira.

Kongamano hili limehudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali, Wadau wa Nishati na wanawake kutoka sehemu mbalimbali hapa Nchini
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango akizungumza na Wadau mbalimbali walioshiriki kongamano la Nishati Safi ya Kupikia lililofanyika leo katika Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete (JKCC) jijini Dodoma. Kongamano linalokwenda pamoja na ugawaji wa mitaji na vitendea kazi vya Nishati Safi ya Kupikia.
NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt Doto BITEKO akizumza na wadau mbalimbali katika Kongamano hilo


No comments:

Post a Comment