Na Okuly Julius - Dodoma
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uthibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Dkt. James Andilile amesema mamlaka hiyo ina wajibu wa kutekeleza ili kuhakikisha inamtua Mama kuni kichwani.
Dkt. Andilile ametoa kauli hiyo Leo Machi 9,2024 Jijini Dodoma, wakati akizungumza na waandishi wa habari katika banda la Mamlaka hiyo kwenye Kongamano la wanawake la kugawa mitaji na vitendea kazi vya nishati safi ya kupikia.
Dkt. Andilile amesema wajibu wa Mamlaka hiyo upo katika maeneo mawili ambapo ni kuhamasisha uwekezaji katika eneo la nishati safi ya kupikia kwa kuhakikisha kuwa wanatoa vibali au leseni kwa wakati kwa wawekezaji kusudi kwamba waweze kuwekeza.
Pili Mamlaka hiyo inaangalia suala la upatikanaji wa nishati hizo katika maeneo mbalimbali na kuwaeleza wawekezaji wazipeleke hasa maeneo ya vijijini na suala la bei rafiki ili kila mmoja aweze kumudu kununua.
"Tunaamini kama vile serikali ilivyofanikiwa katika eneo la kumtua Mama ndoo kichwani ndio hivyo hivyo tutakavyofanikiwa kumtua Mama kuni kichwani," amesema Dkt.Andilile
Amesema wananchi wengi bado wanatumia nishati ambayo sio safi ya kupikia na madhara katika maeneo mbalimbali ikiwemo afya,upotezaji wa Muda na kuchelewesha Maendeleo kwani wanawake wengi hasa vijijini wanatumia muda mwingi kutafuta kuni badala ya kufanya shughuli zinazoweza kuwaingizia kipato.
"Ukimwezesha mama kupata Muda mwingi wa kufanya shughuli za maendeleo kivyovyote vile familia itaendelea,jamii itandelea na taifa kwa ujumla,"ameeleza Dkt. Andilile
No comments:
Post a Comment