JAMII YAASWA KUZINGATIA ULAJI MZURI KUEPUKA HATARI YA KUPATWA NA TATIZO LA FIGO - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, March 14, 2024

JAMII YAASWA KUZINGATIA ULAJI MZURI KUEPUKA HATARI YA KUPATWA NA TATIZO LA FIGO


Jamii imeaswa kuzingatia utaratibu mzuri wa ulaji ikiwemo kupunguza vyakula vyenye wanga kwa wingi, chumvi, mafuta pamoja na kufanya mazoezi ili kujilinda na kupata magonjwa ya moyo, shinikizo la damu na kisukari, ambayo hupelekea hatari ya kupatwa na tatizo la figo.

Hayo yameelezwa hii leo jijini Dodoma na Daktari Bingwa wa magonjwa ya ndani kutoka St. Camillus Hospital Dkt. Bonaventura Mpondo wakati akizungumza na waandishi wa habari ikiwa ni maadhimisho ya siku figo duniani.

Dkt Mpondo amesema takwimu zinaonesha kuwa magonjwa ya moyo, shinikizo la damu na kisukari ndiyo yanayoongoza kwa kusababisha tatizo la figo ambapo ameiasan jamii kupima afya zao mara kwa mara ili kutambua magonjwa hayo mapema.

Aidha ameshauri jamii kufuata masharti ya kitaalam juu ya matumizi sahihi ya dawa kwa wale wanaogundulika kuwa na magonjwa hayo pamoja na matibabu yasiyo ya dawa ambayo ni mtindo bora wa maisha (lishe bora,ufanyaji wa mazoezi) ili kuzilinda figo zao.

Ameongeza kuwa mgonjwa wa figo ambaye tayari figo zake zimeshaathirika asikate tamaa kwani zipo namna za kitaalam kumsaidia ikiwemo matumizi ya dawa, ushauri wa mpangilio wa lishe usafishaji wa damu au kupandikiza figo pale inapobidi.

Kauli mbiu ya maadhimisho ya figo duniani kwa mwaka huu inasema afya ya figo kwa wote, boresha usawa wa kuifikia huduma na matumizi sahihi ya dawa

No comments:

Post a Comment