Machi 12, 2024 Katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni imefunguliwa kesi ya Jinai Namba (Cc.6600) dhidi ya Bw. BENJAMIN CHALRES CHUMA kwa mashtaka ya kuomba na kupokea RUSHWA kinyume na kifungu cha 15(1)(a) na 15(2), cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa [CAP 329 RE 2019]
Mshtakiwa akiwa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kilungule Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, aliomba Rushwa kiasi cha shilingi 120,000 na kupokea kiasi cha shilingi 100,000 ili asimchukulie hatua za kisheria Bw. YUREDI MTESELI RWEBUGISA.
Mshtakiwa alisomewa mashtaka yake mbele ya Mheshimiwa ERICK RWEHUMBIZA na alikana makosa yote. Shauri limepangwa tena tarehe 28/03/2024. TAKUKURU- KINONDONI.
No comments:
Post a Comment