Na. Asila Twaha, Mwanga
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) imeuagiza uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga kuhakikisha inakamilisha ujenzi wa Hosptali ya Wilaya pamoja na kituo cha afya Kirya katika halmashauri hiyo.
Kaimu Mwenyekiti wa Kamati Mhe. Ester Bulaya (Mb) amesema hayo Machi 22, 2024 baada ya kukagua miradi hiyo na kutoridhishwa utekelezaji wa miradi hiyo ambayo mpaka sasa imekamilika kwa asilimia 50.
Amesema Serikali imewekeza fedha nyingi kwenye miradi hiyo lakini Halmashauri hiyo bado inasuasua utekelezaji wake ambapo baadhi ya majengo bado hayajakamilika
wakati ilishapewa zaidi sh. bilioni 2.
"Halmashauri nyingine wamepewa 1.8 wapo katika hatua nzuri ya utekelezaji na kuna majengo yameshakamilika na mengine yameanza kutumika kutoa huduma ila Halmashauri ya Mwanga haijakamilisha" amesema
Ameendelea kuhoji kuwa taarifa inasema kuna vifaa stoo vya zaidi ya shs. milioni 200 na hakuna hata jengo moja lililokamilika kwa asilimia 100 ” ameuliza Mhe. Bulaya
Pia amekerwa kutokufuatiliwa kwa vifaatiba na dawa MSD na Serikali ilishatoa pesa shs. bilioni 1.1 " tumesikia hivi karibuni vimefika vifaa vya milioni 100 tu kisa mmesikia Kamati inakuja ” watendaji timizeni wajibu wenu” amewasisitiza
Naye Mhe. Michael(Mb) akisoma mapendekezo kwa niaba ya Kamati imeiataka Ofisi ya Rais -TAMISEMI kabla hawajatoa na kushughulikia fedha walizotakiwa waongeze kwa Halmashauri sh. milioni 300 kwanza wafanye tathmini na ufuatiliaji wa kiasi cha fedha ambacho kishatumika zaidi ya sh. bilioni 2 katika kutekeleza mradi huo.
Kamati pia imemtaka CAG afanye uhakiki wa vifaa vilivyopo stoo vya kiasi cha shs. milioni 202 na kuwasilisha taarifa kwa Kamati kabla ya tarehe 28 Machi, 2024, Kamati imemtaka Mkurugenzi awasilishe taarifa kwa CAG kwa ajili ya uhakiki kibali cha Ofisi ya Rais – TAMISEMI kilichoiruhusu Halmashauri kutekeleza mradi kinyume na miongozo ya utekelaji wa mradi wa hospitali ya Wilaya.
Aidha, pamoja na mapendekezo mengine Kamati imemtaka Mkurugenzi kufuatilia dawa na vifaa tiba ambavyo malipo yake yashalipwa MSD.
Mhe. Bulaya amewataka watumishi kutokuvunja sheria kwa kujiamulia mambo bila kufuata taratibu kwa kutekeleza wakati wanatekeleza miradi na kuwaeleza kama kuna uhitaji wa kufanya mabadiliko wafuate utaratibu wa kuomba kibali Ofisi ya Rais -TAMISEMI huku akimuelekeza Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI vibali vinapoombwa vijibiwe mapema ili kazi ziende kwa haraka.
No comments:
Post a Comment