MAJALIWA ASISITIZA ‘FOMU YA URAIS NI MOJA’ - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Sunday, March 10, 2024

MAJALIWA ASISITIZA ‘FOMU YA URAIS NI MOJA’


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameongoza uchangishaji wa fedha kwa ajili ya kumuwezesha Rais Dkt. Samia kuchukua fomu ya kugombea Urais mwaka 2025.

Fedha hizo zimechangwa wakati wa mkutano wa Wanawake wa kumpongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwa Kinara wa Nishati Safi ya kupikia, Mazingira na Afya ya Mama na Mtoto.

Fedha hizo kiasi cha Shilingi Milioni 5, zimekabidhiwa kwa Waziri Mkuu na Waziri wa maendeleo ya Jamii, Jinsia na Makundi Maalum Mhe. Doroth Gwajima kwa niaba ya wanawake hao.


📍 Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam
🗓️ Machi 10, 2024

No comments:

Post a Comment