WAZIRI NDEJEMBI AWASILI MOROGORO KUSHIRIKI KONGAMANO LA NISHATI SAFI YA KUPIKIA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, March 17, 2026

WAZIRI NDEJEMBI AWASILI MOROGORO KUSHIRIKI KONGAMANO LA NISHATI SAFI YA KUPIKIA


Waziri wa Nishati, Mhe.Deogratius Ndejembi akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Adam Malima mara baada ya kuwasili mkoani Morogoro kushiriki Kongamano la Nishati Safi ya Kupikia.

Kongamano hilo limehusisha Wizara na Taasisi mbalimbali za Umma kutoka Tanzania Bara na Zanzibar pamoja na wadau mbalimbali zikiwemo taasisi za fedha pamoja na wazalishaji, wasambazaji na watumiaji wa nishati safi ya kupikia.

Kongamano limeandaliwa na Wizara ya Nishati kwa kushirikiana na Taasisi ya Uongozi likiwa na kaulimbiu ya Kuimarisha Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia kwa Maendeleo Endelelevu

Kutoka Wizara ya Nishati, Mhe. Ndejembi ameongozana na Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Nishati (Umeme na Nishati Jadidifu), Bw.Nolasco Mlay.

No comments:

Post a Comment