MHANDISI LUHEMEJA- AWAPONGEZA WATUMISHI OFISI YA WAZIRI MKUU KWA MSHIKAMANO KAZINI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, March 13, 2024

MHANDISI LUHEMEJA- AWAPONGEZA WATUMISHI OFISI YA WAZIRI MKUU KWA MSHIKAMANO KAZINI


Na Mwandishi Wetu: Dodoma

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhandisi Cyprian Luhemeja amewapongeza watumishi wa Ofisi hiyo na Taasisi zilizo chini ya Ofisi hiyo kwa mshikamano wanaokuwa nao  katika kutekeleza majumu yao.
 
Ameyasema hayo wakati wa hafla fupi ya iftar aliyoandaa kwaajili ya watumishi walio chini ya ofisi yake pamoja na taasisi zake kwa lengo la kukaribisha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani pamoja Mwezi Wa Kwaresma iliyofanyika tarehe 12 Machi, 2024 jijini Dodoma.

Aidha, amesisitiza kuwa ni wajibu wa kila mfanyakazi kuelimisha jamii kuhusiana na utekelezwaji na utendaji unaofanywa na ofisi hiyo iliwaweze kutambua kazi zinazo fanywa.

Pia amewasihii kujikita katika kusaidia jamii kwenye sekta ya Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu ili kuweza kutatua changamoto zinazotokana na sekta hizo.

No comments:

Post a Comment