Raia huyo wa Zimbabwe alitumia mtandao wa kijamii wa Instagram Alhamisi asubuhi kuwashukuru uongozi wa klabu na mashabiki kwa sapoti yao katika kipindi chake cha miaka minne katika klabu yenye maskani yake Chamazi.
“Ni kwa hisia tofauti natangaza kuachana na Azam FC. Miaka hii minne imekuwa safari ya ajabu, iliyojaa changamoto, ushindi na kumbukumbu nzuri.
“Nataka kutoa shukurani zangu za dhati kwa kila mtu anayehusishwa na klabu, kuanzia uongozi hadi wakufunzi, wachezaji wenzangu na muhimu zaidi, mashabiki.
“Ninapoendelea na sura mpya katika maisha yangu ya soka, huwa nabeba mafunzo niliyojifunza wakati nikiwa Azam FC, sapoti niliyoipata kutoka kwa mashabiki imekuwa ya kushangaza na nitahifadhi kumbukumbu tulizo nazo milele.
“Naamini nguvu na uwezo wa klabu hii na sina shaka kwamba itaendelea kupata mafanikio makubwa.
“Nawatakia Azam FC, wachezaji wenzangu, makocha na mashabiki wote mafanikio na furaha duniani.
"Asante kwa safari ya ajabu," anaandika.
No comments:
Post a Comment