Mmiliki tajiri wa vyombo vya habari Robert Murdoch amemchumbia mpenzi wake, timu yake imethibitisha.
Mzee huyo mwenye umri wa miaka 92 ameripotiwa kuwa anachumbiana na mwanabiolojia mstaafu wa Urusi Elena Zhukova, 67.
Ndoa hiyo inayotarajiwa kufungwa katika shamba lake la Moraga huko California mwaka huu, itakuwa ni uchumba wa tano lakini wa sita kwa Bw.Murdoch.
Alijiuzulu kama mwenyekiti wa Fox na News Corp mwaka jana.
Kulingana na gazeti la New York Times, ambalo lilitoa habari hiyo, harusi hiyo imepangwa kufanyika Juni na mialiko tayari imetumwa.
Wawili hao wanasemekana kukutana kwenye tafrija iliyoandaliwa na mmoja wa wake zake, mjasiriamali mzaliwa wa China Wendi Deng.
Wenzi wengine wa zamani wa Bwana Murdoch walikuwa mhudumu wa ndege wa Australia Patricia Booker, mwandishi wa habari mzaliwa wa Scotland Anna Mann, Bi Deng na mwanamitindo na mwigizaji wa Marekani Jerri Hall.
Ndoa ya awali ya Murdoch a Jerry Hall ilimalizika kwa talaka mnamo 2022 baada ya miaka sita ya ndoa yao.
Murdoch ni mmiliki wa vyombo vya habari kama Sky, Fox, Fox Entertainment Group, Sky Italia na vingine vingi na kwa mujibu wa Forbes yeye ni tajiri namba 71 Duniani.
No comments:
Post a Comment